Habari za leo ndugu msomaji. Ni matumaini yangu umemaliza vyema weekend yako. Leo ni jumatatu nyingine tena ambayo tunakwenda kuongeza uzalishaji wetu karibu sana.


Jana nilihudhuria kanisani nikakutana na Ushuhuda wa ajabu sana. Mtoto mdogo alieko shule ya msingi aliamua kwenda shule kwa miguu siku zote ili nauli yake akatoe kwa watoto yatima.  Nauli ya mwanafunzi ni kama tsh 200 tu lakini mtoto huyu aliamua aikusanye kila siku ili aweze kuwapa kitu watoto yatima. Inawezekana wewe unapata kipato kikubwa sana lakini unashindwa kujua ujiwekee bajeti ya aina gani ili uweze kutoa.

Kutoa ni tabia ambayo tunajiwekea na wala sio kua na pesa nyingi. Kutoa ni moyo sio utajiri haijalishi unapata kipato kidogo kiasi gani bado unaweza kutoa na kuwasaidia wengine. Vile vile usisubiri hadi uwe na pesa nyingi ndio useme utaweka bajeti ya kutoa msaada kwa wengine. Anza leo jijengee tabia hii maana ina Baraka za kipekee katika lile unalolifanya.

Kutoa kunakuletea ulinzi
Unapojijengea tabia ya kutoa unajiwekea ulinzi kazini kwako, kwenye biashara zako na kwenye chochote kile kinachokuingizia kipato. Unapowasaidia watu hua wananena maneno ya Baraka juu yako na mali zako. Huvyo unajikuta upo kwenye ulinzi bila hata kujilinda. Kuna wakati unaweza kupitia changamoto nyingi lakini ukazivuka kirahisi kwasababu ya tabia yako ya utoaji. Mungu anaondoa yale mabaya ambayo yangekuja juu yako ili uweze kuendelea kuwasaidia wengine.

Kutoa kunaleta ongezeko.
Kutoa kunafanya ongezeko katika kile unachokifanya. Kwa kupitia tabia ya utoaji unaongezewa kingi Zaidi kama ni biashara yako unakuta inakua na kupanuka sana kwasababu ya tabia yako ya utoaji. Haijalishi umetoa kiasi gani lakini kama ulitoa kwa moyo utaona ongezeko pale ulipotoa.

Kutoa kunafungua njia.
Utoaji hufungua njia mbalimbali za mafanikio katika maisha yako. Kwa kupitia tabia ya utoaji utaona mambo makubwa yakifunguka ndani ya maisha yako. Kama upo shuleni utajikuta ufaulu wako unaongezeka vikwazo vya namna mbalimbali vinakwenda kuondoka.

Kumbuka: Hatutoi kwakua tuna vingi tunatoa kwasababu ni tabia tuliyoamua kuiishi. Utoaji mzuri ni ule unatoa halafu unasahau. Usitoe halafu unasubiria uone matokeo ya utoaji wako. Kutoa ni kama kupanda mbegu katika mashamba ambayo huyamiliki hivyo mavuno yakitokea yanakufikia wewe hata bila kujua ulipanda wapi.

Nikutakie week njema yenye matokeo bora.
Nguvu Ya Tabia
0654726668
jacob@jacobmushi.com
Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading