Katika maisha yetu kila siku tuna watu wanaofanya kazi kwa bidii sana kila siku kwenye ajira zao, kwenye biiashara zao, kwenye vipaji vyao na kadhalika. Kitu  kinanachowatofautisha watu hawa mara nyingi ni matokeo ya kile wanachokifanya. Kila mmoja atapata kutokana na alichokitoa. Mara nyingi nikikutana na watu wengi hua napenda kuwauliza swali hili, “Ni kitu gani hasa kinachokufanya wewe uwe unaamka asubuhi na mapema na kwenda kazini kwako na kufanya kazi? Kila mmoja ana jibu lake la tofauti mwingine atakwambia ni watoto, mwingine atasema anatafuta maisha mazuri, kitu kinachonisikitisha sana utakuta mtu anakwambia “wasingekua hawa watoto hii kazi ningeshaiacha nafanya tu ili wanangu waishi”
Kama kuna kitu cha muhimu cha kungundua ni kufahamu kwa hakika ni kitu gani kimekuleta hapa duniani na ukifanyie kazi hujaja duniani kulea watoto, hilo ni jukumu tu na sio kusudi la wewe kuja hapa duniani. Ipo sababu ya pekee ambayo Mungu amekuleta kipindi hiki na sio kipindi kingine kilichopita kuna thamani unatakiwa uiache hapa duniani.
Utawezaje sasa kufahamu kile ulichokusudiwa kukifanya duniani?
Fanya kile unachokipenda.
Kama kuna kitu cha muhimu kufanya kwenye  hii dunia na kikuletee furaha kila siku ni kufanya kile unachokipenda kwa maana hiki kinatoka ndani ya moyo wako huwezi kuchoka kufanya. Utawezaje kugundua kile unachokipenda? Tafuta muda ukiwa peke yako na tafakari kwa sana ni kitu gani unatamani siku ukiondoka hapa duniani uache kikisemwa uache watu wakikizungumzia ukiweza kufanya hivyo utagundua kusudi la wewe kuwepo duniani. Tafadhali sana kama bado hujagundua kusudi fanya zoezi hili leo.
Tengeneza mwisho wako.
Tengeneza mwisho unaoutaka kwenye kile unachokipenda kukifanya,, kama ni kipaji  jione mahali unapotaka kufika kabla hujafika kama ni biashra ione ikiwa imefika mahali ambapo hata ukiondoka duniani utaondoka ukiwa na furaha ya kukamilisha ulichokianza. Kwa lugha nyingine tunasema uwe na maono kwenye kile unachokifanya unajiona wapi miaka 10 au 20 ijayo kwenye hiyo kazi yako, biashara au kipaji chako. Ukiweza kutengeneza kitu kama hichi utaweza kua na mfumo wa maisha ambao utakuletea furaha kwa kua unajua mahali unapoelekea na pia huwezi kuchukuliwa na upepo wowote. Haiwezekani tu mtu akaja akakwambia kuna nafasi za ajira zimetoka na wewe ukakimbilia huko wakati umeshaelewa ni kitu gani unafanya.labda kama ajira hiyo inakupelekea kule unakotaka kufika.
Fanya kwa bidi na maarifa.
Kile ulichokigundua kwenye maisha yako na ukaweza kujitengenezea mwisho mzuri unaoutaka kifanye kwa bidii na maarifa, jifunze kila siku juu ya kile unachokifanya. Ongeza ujuzi ambao hakuna mtu mwigine anao, soma vitabu ambavyo hakuna alievisoma fikiria namna ya tofauti. Ukweli ni kwamba huwezi kupata vile vitu unavyovitaka kwenye maisha yako kama utabakia ulivyo sasa hivi, nikiwa na maana kwamba kama hutaongeza ufahamu Zaidi ya huo ulio nao sasa hivi hata matokeo ya unachokifanya yatabaki vile vile hayatakua na tofauti yeyote.
Jifunze kila siku.
Ukitaka ubora kwenye hicho uanchokifanya kila siku unatakiwa ujifunze kila siku kuza ufahamu wako kwa kusoma vitabu vya kuhamasisha, kusoma Makala kwenye blogu kama hii, utaona matokeo bora kwenye kazi yako. Kitu cha muhimu cha kufahamu ni kua na nidhamu mafanikio makubwa yanamuhitaji mtu mwenye nidhamu mtu ambaye anasema nitaaamka saa kumi ya usiku kila siku nijifunze na akafanya hivyo kama umechagua kua mtu mkuu na anaetaka kuacha alama duniani uanhitaji
kujifunza kila siku.
Hujachelewa bado.
Hujachelewa kua yule mtu uliekua unatamani kua haijalishi una miaka mingapi sasa kwa sababu tu upo hai unayo nafasi ya kufanya mambo makubwa na kuacha alama. Na wakati sahihi ulikua ni jana ila wakati mwingine sahihi Zaidi ni leo anza leo usikate tamaa changamoto zipo kila mahali ni kubadili mtazamo juu ya zile changamoto unazozipitia tu.
©Jacob Mushi 2016
Niandikie 0654726668
Email jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading