Watu wamekuwa wanasema mwanzo ni mgumu ni kweli kuna baadhi ya mambo mwanzo ni mgumu. Ila bado kuna mambo ambayo ni rahisi sana kuanza ila kumaliza vile ambavyo unataka ndio imekuwa changamoto ya wengi. Unaweza kuwa na mawazo makubwa na mipango mikubwa wakati unaanza mwaka lakini unapofika mwisho unajikuta hujafanya hata robo ya kile ambacho ulikipanga na kuanza.

Mambo mengi unayakuta ulianza na kuishia nusu nus utu. Mchakato upo katikati kuelekea kwenye ushindi.

Haijalishi umeanzaje iwe ni kwa ugumu au kwa urahisi cha muhimu ni unamalizaje? Umefikia malengo uliyopanga kwa kiasi gani? Umeweza japo kuvuka nusu ya mipango yako?

Usiwe mwepesi sana kuanza jambo ambalo hutaweza kufika nalo mwisho, haina maana yeyote kuingia kwenye jambo ambalo hutafika mwisho wa vile ambavyo umepanga. Kabla hujaanza kitu hakikisha kabisa kwamba umeamua na utajitoa vya kutosha hadi uweze kufikia ule mwisho unaoutaka.

Kuna mengi yatatokea katikati lakini kikubwa ni wewe kuendelea kushikilia lile kusudi la wewe kuanza. Endelea kuamini kwamba inawezekana.

Kumaliza kwa ushindi ndio kila mmoja anataka, kumaliza ukiwa umetimiza kile ambacho ulipanga hiyo ndio furaha ya kila mmoja. Ili uweze kufika mwisho hivyo inakupasa uwe umejitoa kwa uhakika kabisa kwamba lolote litakalotokea nipo tayari kukabiliana nalo.

Usikubali kuisaliti ndoto yako, unajua kwamba kuishia njiani ni kuisaliti ndoto yako? Unajua kukata tamaa ni sawa na kumuacha mpenzi wako aliekuwa anakupenda sana halafu eti kwasababu tu ya changamoto? Usikubali kuliacha kusudi la Mungu ndani yako, hilo lipo ndani yako siku zote za Maisha yako.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading