Ukimuuliza mtu akutajie mambo 3 ya muhimu sana kwenye Maisha yake ni wachache wataweza kukujibu kwa usahihi nikiwa na maana kwamba walikuwa wanayajua kabla hujawauliza. Ni rahisi mtu kujibu kwa kutamka kile ambacho kitamjia kichwani kwa wakati huo lakini ukweli ni kwamba utakuta hafanyi chochote katika hayo aliyosema ni ya muhimu kwenye Maisha yake.

Embu jiulize sasa hivi unayafahamu mambo matatu ya muhimu sana kwenye Maisha yako kuliko mengine? Kama bado hujayajua basi unahitaji msaada Rafiki yangu, kama unayajua lakini leo unaposoma hapa hujafanya hata moja basi sio ya muhimu.

Mfano rahisi unaweza kusema mimi ni AFYA, FAMILIA NA PESA. Yaani kila siku nitahakikisha nakuwa na afya bora kwa kula vizuri, kufanya mazoezi, kusoma vitabu, kusali (kwasababu kuna afya ya kiroho, kiakili na kimwili). Vilevile nitahakikisha ninapata muda wa kuwa karibu na familia yangu kila siku (kila mmoja ana watu anaowajali sana na kuwapenda hawa ndio familia yako). Tatu ni fedha, ni lazima nihakikishe kila siku naingiza fedha au nafanya jambo ambalo litakuwa ni chanzo cha mimi kuwa vizuri kifedha (huenda ni biashara, ajira, kipaji au chochote).

Unaweza kusema mbona hujataja furaha? Furaha ipo ndani ya vitu hivyo vyote vitatu. Kama huna afya bora huwezi kuwa na furaha sawa na mtu alie na afya bora. Huna familia huna yeyote unaemjali huwezi kuwa na furaha, huna pesa, huna chanzo chochote cha mapatoa utakuwa unateseka tu hapa duniani labda uwe mtoto mdogo. Hivyo furaha inajengwa na vile vipaumbele vyetu vya Maisha.

Ukiwa na vipaumbele vikubwa vya Maisha unapata nafasi ya kuweka malengo makubwa kwenye vipaumbele hivyo. Malengo hayo yanaweza kuwa ya miaka 50, 20, 10, 5, na 1 au yanaweza kuwa ya mwezi, wiki na siku.

Rafiki yangu jitahidi ujue vitu vya muhimu sana kwenye Maisha yako ili uwe unavifanyia kazi kila siku na uweze kuvipata. Unajua huwezi kupata kitu ambacho hujui kama unakitaka eeh, na hata ukikipata unaweza usitambue kwasababu hakikuwa na umuhimu kwako.

Kama unakwama ninaweza kukusaidia nimeamua kukusaidia angalau kwa wiki moja uweze kutengeneza vipaumbele vyako vya Maisha na uwe unavifanyia kazi kila siku. Bonyeza link mwishoni mwa Makala hii uweze kufuata maelekezo.

 

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

2 Responses

  1. Ubarikiwe Sana kaka masomo yako yaninibariki Sana, nakupenda rafiki yangu. Ahsante Sana kwa elimu hii unayonipa

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading