Habari Rafiki, unajua matatizo mengi uliyonayo yanasababishwa na ukosefu wa fedha za kutosha. Na kinachosababisha haya yatokee kwako ni wewe pale unapokosa vitu vichache sana vya kufanyia kazi.

Leo nakwenda kukuonesha suluhisho la tatizo lako la kutokufikia malengo ya kifedha. Ni kweli inawezekana kabisa Januari yam waka 2021 ikawa njema Zaidi kwako kwasababu tu utaweza kufanyia kazi hiki ninachotaka kukuelekeza leo.

Jifunze kwenye nukuu hii Too many people spend money they earned..to buy things they don’t want..to impress people that they don’t like. –Will Rogers. (Watu wengi sana wanatumia pesa wanazopata kununua vitu wasivyovitaka na kuwavutia watu wasiowapenda wala kuwahitaji)  Utakubaliana na mimi kwamba wapo wengi wanaweka akiba ya fedha ili kuja kuzitumia vizuri mwisho wa mwaka.

Utakubaliana na mimi pia wapo watu wanaweka malengo Fulani ya kukusanya fedha lakini inapofika katikati ya mwaka anajikuta amekwenda kununua vitu ambavyo wala hakuwa amevihitaji.

Tuseme mfano wewe hujawahi kumiliki Tsh milioni moja, mwaka huu ukajiwekea malengo ya kukusanya fedha yaani kuweka akiba. Kufika mwezi wa saba hivi ukawa tayari umefikisha milioni. Ukweli ni kwamba kwasababu ile pesa haina usimamizi mzuri ni rahisi sana kuingiwa na tamaa na kwenda kuitoa kununua vitu Fulani vizuri vizuri.

Kuna mahali nilisoma, jamaa alijikusanya kwenye kibubu mpaka ikafika milioni tatu. Sasa akaingia na tamaa akavunja kibubu akaenda kununua Iphone 11 Pro. Siku kadhaa mbele Katika kutembea tembea pale Ubungo wahuni wakamkwapua ile simu.

Soma: Sehemu 3 Muhimu sana za Kuwekeza kwenye Maisha Yako Kila Siku.

Nikwambie ukweli, ukikusanya pesa bila ya malengo, utaitumia bila ya malengo, ukikusanya pesa ukiwa na malengo na ukaiweka sehemu ambayo ni rahisi wewe kwenda kuitoa utaishia njiani. Ukikusanya pesa pia bila ya kuwa na mtu anaekukumbusha kuna mahali utafika utaacha kukusanya.

Hizi ndio njia ya Kutatua matatizo haya matatu ambayo yanawakumba wengi.

a/ Hakikisha una Malengo Makubwa na ya Muda mrefu.

Ndio kama huna malengo ya Makubwa nay a muda mrefu ukiwekeza fedha utafika katikati na kusema ngoja nikachukue pesa zangu. Ukibanwa na shida Fulani utajikuta umekwenda kuzitoa huko zote. Malengo makubwa na ya muda mrefu yatakusaidia wewe kutokutumia pesa zako zote mwisho wa mwaka kwasababu tu ulizikusanya.

b/ Wekeza Pesa Sehemu ambayo Huwezi Kuifikia Kirahisi.

Hapa kama unaweka akiba basi usiweke kwneye kibubu ambacho unaweza kukivunja wakati wowote. Kwasababu pesa inaweza kuwa nyingi ambayo hujawahi kuimiliki kwa wakati mmoja na utaingiwa na tamaa.

Usiweke kwenye bank account ambayo una card na pia umeunganisha na sim banking. Hii itakuwezesha kuvishinda vishawishi vya kujikuta umeitoa pesa. Unapokumbwa na matatizo Fulani ya pesa ile hela iliyoko karibu yako ndio huwa ya kwanza kutumika, sasa kama wewe unaweka akiba karibu yako lazima utajikuta umeitumia kwenye matatizo.

Wekeza kwenye mifuko ya uwekezaji kama UTT AMIS, Wekeza kwenye sehemu ambayo unajua kabisa huwezi kuifikia kwa haraka.

c/ Nipe Kazi ya Kukumbusha

Ndio njia ya tatu ya kutatua matatizo yote ni unipe mimi kazi ya kukusaidia kukufuatilia kwenye lengo lako la kuwekeza hadi litimie. Unakuja kwangu na malengo yako makubwa, na njia ile ambayo umeamua kuwekeza fedha zako halafu kazi yangu inakuwa ni kuhakikisha unawekeza fedha ila kila mwezi. Mimi nitahakikisha nakukumbusha kila mwezi ili utimize lengo lako bila kuingiwa na vishawishi.

Karibu Sana

Rafiki Yako

Jacob Mushi

2 Responses

Leave a Reply to Jacob MushiCancel reply

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading