Tanakutana na vitu vingi sana katika maisha yetu ya kila siku, tunakutana na changamoto mbali mbali kwenye kila tunachokifanya. Watu wengi wanapopitia matatizo wanaishia kulalamika na kulaumu mwisho wa siku matatizo ndio yanakua mengi Zaidi. Leo ningependa tujaribu kubadili mtazamo wetu juu ya kila kitu tunachokutana nacho kiwe kizuri au kibaya jaribu kukiangalia kama fursa.

Jiulize kwenye hili tatizo ninalopitia ninaweza kujifunza kitu gani? Badala ya kulalamika na kulaumu tafuta kitu cha kujifunza, angalia namna unavyoweza kufaidika wewe mwenyewe kwenye tatizo unalopitia. Kama umelala njaa jana unatakiwa usilaumu na kusema maisha magumu jifunze kuweka akiba. Kama umefukuzwa kazi usilalamike na kuona kama ni mwisho wa dunia jaribu kuona kuna kazi mpya inakuja na itakuletea uzoefu, mshahara mkubwa Zaidi, utakutana na watu wengine wazuri Zaidi. Unaweza kutumia mtazamo huu kwenye tatizo lolote unalopitia JIULIZE NINAWEZAJE KUFAIDIKA KWENYE TATIZO HILI NINALOPITIA?

Tuna kutana na watu wengi na wa namna mbalimbali kila siku, ulishawahi kujiuliza unawezaje kunufaika na fursa hii? Kitu cha ajabu ni kwamba wau wengi hawajalitambua hili, kila mtu unaekutana nae kwenye maisha ana kitu kipya kwa ajili ya maisha yako, kuna kitu unaweza kujifunza kwake, kuna fursa unaweza kuipata kwake, mara nyingi nimekua nakutana na watu wengi, nikagundua tuna matatizo makubwa sana, watu wanawaza mbaya tuu juu ya wengine. Huwezi kujua unaekutana nae leo anaweza kuleta kitu gani kipya kwenye maisha yako, unaweza kukutana na mtu akawa sababu ya maisha yako kubadilika. Anaweza kuleta mawazo mapya kwenye maisha yako.

When we clearly understand that there is no superior sex
or superior race, we will have opened the door
of communication and laid the foundation
for building winning relationships with
all people in this global world of ours.

Kila mmoja wetu akitambua kwamba hakuna alie bora Zaidi ya mwenzake na anaweza kujifunza kitu kwa mtu yeyote anaekutana nae tutaweza kufungia milango ya mawasiliano ambayo itasababisha tuweze kushinda kwenye mambo mengi sana, ukitambua kila mtu unaekutana nae ana kitu cha kipekee ambacho wewe huna utakua makini ili uweze kujifunza kitu kwake. Ukitambua pia kila unaekutana nae anafahamu kitu ambacho wewe hukifahamu maana kila mmoja ameishi kwenye mazingira ya tofauti na ameishi na watu wa tofauti hivyo kila mmoja wetu ana kitu cha kipekee kwa ajili ya mwenzake.

Ni wakati wa kujiuliza ninawezaje kufaidika na huyu mtu niliekutana nae leo?, ninajifunza nini kwenye tatizo hili ninalopitia?

Asante sana na Karibu.
Tunaweza kuwasiliana kwa 0654726668 E-mail jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading