Pale unapohisi.

jacobmushi
By jacobmushi
1 Min Read
Pale unapojihisi kukata tamaa ndio sehemu hasa ya kuongeza bidii maana ni matokeo yanavyokwenda kuonekana.

Pale unapojihisi kuchoka ndio wakati wa kuinuka tena kwani vita ndio imeanza mapambano ndio yamechanganya uchague kurudi nyuma upotee kabisa au upambane hadi mwisho.

Pale marafiki zako wanapokucheka na kukwambia umepotea ndio wakati hasa wa kuonyesha unajiamini na unakiamini vyema kile unachokifanya.

Pale watu uliotarajia wakupe msaada wanapokua sababu ya wewe kukwama sio wakati wa kulalamika bali ni wakati wako wa kukomaa na kujifunza kusimama mwenyewe.

Pale unapoona kabisa mambo yamekua magumu ndio wakati wenyewe wa kuonyesha uwezo wako ulionao kwenye kufanya vitu vitokee.

Unaweza kubadili kila hali unayoiona kwenye maisha yako kwenye biashara. Badili mtazamo wako sasa.

Upopitia changamoto yeyote ndio wakati wa kung’ara kwani ukiishinda changamoto ile hauwi mtu wa kawaida tena. Unapanda viwango.

Asante sana
Jacob Mushi
Mawasiliano 0654726668 Email jacob@jacobmushi.com

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading