By Mushi Jacob. 

Kitu chochote kilichopita kimeshapita. Kiwe kizuri au kibaya kimeshapita. 

Kwanini nasema hivyo? Watu wanajikuta wanarudi nyuma Kwasababu ya mambo yaliyopita. Inawezekana mambo haya ni mazuri sana pia yakakurudisha nyuma. 

Wana wa Israel walipopitia magumu ya Jangwani wakaanza kukumbuka masufuria ya nyama na pilau waliokuwa wanakula bure. 

Unapoacha kazi ukaamua kwenda kujiajiri ukipitia changamoto ngumu za maisha unaweza kuanza kukumbuka yale mambo mazuri uliyokuwa unapata kwenye ajira. 
Uhakika wa kipato. 
Ulikua unaweza kukopa na ukawa na uhakika wa kupata pesa mwisho wa mwezi. 
Hivyo haya mazuri yanaweza kuwa sababu ya wewe kuacha kuifikia ndoto yako. 

Mara nyingi tunadhani ni mambo mabaya tu ndio huwarudisha watu nyuma kumbe hata mazuri. Unapoamua kwenda kujitegemea umeondoka Nyumbani ambako ulikuwa na uhakika wa kula kila siku uwe na pesa usiwe nayo utakula. Lakini sasa upo kwako ukikosa pesa walala njaa. Unaweza kuana kufikiri kurudi kule ulipotoka. 

Umekuwa na mpenzi mpya akafanya mambo ambayo sio Mazuri kama yule mpenzi wako wa zamani aliokuwa anakufanyia. Labda zawadi huyo aliekuacha alikuwa anakupa vitu vya thamani sana kuliko huyu ulienae sasa. Ulikua una uhakika wa pesa pale unapomwomba (wadada) huyu wa sasa labda ndio anapambana kutafuta maisha. Kumbukumbu ya mpenzi wako wa nyuma inaweza kukusababisha ukatamani tu umrudie bila kujali aliyokufanyia. Hii nina uhakika nayo kabisa. 

Past is always the past forget about it. 

Unaweza ukatamani bora niwe nae tu hata kama ana mwingine Kwasababu nna uhakika wa pesa za matumizi. Lakini vipi kuhusu maisha yako ya baadae? Vipi kuhusu ndoa itakuaje? 

Unaweza kutamani kurudi kwenye ajira Kwasababu ya ugumu wa maisha unayopitia hapa sasa hivi ukasahau jinsi mshahara ulivyokuwa hautoshi. Ukasahau manyanyaso ya pale Kazini, ukasahau jinsi ambavyo ndoto zako hazitakaaa zitimie ukiwa kwenye ajira. 

Past is always the past forget about it. 

Kama ni Zawadi zichome tu.!
Wana wa Israel walikumbuka masufuria ya nyama wakasahau viboko, kutumikishwa kazi ngumu walizopitia. 

Utamu kidogo wa zamani usikufanye usahau magumu yaliyokuwa yanakusonga. 

Hichi unachopitia sasa hivi kitapita. Utafika Kaanani yako. Endelea kuitazama Kaanani yako. Bado kidogo utalimaliza jangwa. 

Ni mimi Rafiki Yako 
Jacob Mushi 
Tembelea www.jacobmushi.com 
Nunua Kitabu Changu kiitwacho Siri 7 za Kuwa Hai Leo. 
+255 654 726 668

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading