Penda Mafanikio ya Wengine

Ukitaka kufanikiwa penda mafanikio ya wengine.

Habari ndugu msomaji wetu ni matumaini yangu unaendelea vyema. Leo tunazungumzia kuhusu mafanikio.
Kila mmoja wetu anatamani kufanikiwa pale mahali alipo.
Nikuulize swali hua unafurahia mafanikio ya wenzako?

Ukitaka kufanikiwa penda mafanikio ya waliofanikiwa. Huwezi kuwa na kitu unachokichukia huwezi kua tajiri kama unawachukia matajiri. Wiki iliyopita nilikua na rafiki yangu mmoja akaniambia kua yeye ni maskini kwa kua matajiri wamechukua pesa zote. Ukiangalia hapo utagundua huyu mtu hawezi kufanya bidii yeyote kwa sababu ya fikra hiyo aliyonayo maana anajenga chuki juu ya waliofanikiwa.

Badilisha mtazamo ulionao juu ya watu wakiofanikiwa utabadilisha maisha yako. Kuna wengine wana imani potofu mtu akiwa na pesa wanasema ni freemason au mchawi au jambazi ukiwa na imani kama hizo huwezi kufanikiwa maana huwezi kwenda mahali unapoona kuna moto. Anza kubadili fikra zako sasa wapende waliofanikiwa penda mafanikio yao na wewe utajua walivyofanya wakafanikiwa utaweza kujifunza kwao.

Kupenda tu mafanikio ya wengine hakutakuletea mafanikio moja kwa moja lazima uanze kuchukua na hatua nyingine kujifunza kile unachokitaka kufanya maishani mwako na pia usikate tamaa.

Nashukuru sana kwa kusoma nami leo.
Nina imani utaanza kuwapenda wote waliofanikiwa na wengine wote.
Ubarikiwe sana.

This entry was posted in USIISHIE NJIANI on by .

About jacobmushi

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *