Habari za leo rafiki yangu mpendwa ni furaha yangu kuona wewe ni mzima na umeweza kusoma ujumbe huu leo. Karibu sana.

Katika maisha jambo linaloleta furaha mara nyingi hua ni pale unapokamilisha jambo ulilolianza. Umeweka malengo yako makubwa na ukaweza kuyafanikisha yote lazima uwe na furaha. Lakini haitakiwi uishie kwenye kufurahi tu kwa maana safari ndio imeanza unapokamilisha lengo moja ndio mwanzo wa kuanza lengo lingine kwa lugha nyingine tunasema “unapopiga hatua moja ni mwanzo wa kupiga hatua Nyingine” kwa hiyo usijisahau kwa mafanikio uliyoyapata ukabaki kwenye level uliyopo unaweza kuwa ni mwanzo wa kuporomoka kwako.

Hatari za kutokupiga Hatua Nyingine.

1. Kupoteza vyote ulivyovipata.
Unapokua umesimama huendi mbele kuna hatari kubwa sana ya kupoteza vyote ulivyovipata. Kwakua kama ni fedha unaitumia kwa hiyo inakwisha pole pole, kama wewe ni muimbaji umetoa album nzuri ikakulipa ukiishia hapo utasahaulika kabisa.

2. Kurudi katika hali ya kawaida kabisa.
Unapokwama katika hatua za maendeleo una hatari ya kurudia hali ya kawaida ile uliyokua nayo mwanzoni na kama ulikua unafanya mambo ambago watu wanakusikiliza au kukuangalia unakosa mvuto kabisa. Unatakiwa ujue kwamba watu wanapenda kile unachofanya hivyo ukiacha kufanya hawawezi kukupenda wewe hawawezi kukufuatilia tena.

3. Msongo Mawazo/Stress
Unapokwama lazima utakua na msongo wa mawazo labda kwa wale ambao hawajajua kama wamekwama kwakua wamejisahau ila pale hali inapoanza kua mbaya unapoanza kuporomoka ndipo hatari hii ya msongo wa mawazo huja.

Faida za Kupiga Hatua Nyingine.

1. Kufurahia maisha
Siku zote unaposonga mbele kule ulipolenga lenga kwenda lazima uwe na furaha utakua na furaha kwa sababu ya kile unachokifanya na kule unapoelekea tofauti na mtu ambaye amesimama akidhani amefika. Mwisho wa safari hii ni kifo kwa hiyo kila siku lazima upige hatua nyingine.

2. Unawainua wengine
Unaposonga mbele unafanyika sababu za wengine kuongeza kasi pia. Unatakiwa utambue kwamba hapo ulipo kuna watu wengi wanakutazama na wanajifunza kupitia wewe na yale unayoyafanya pale unapokua unasonga mbele unakua ni hamasa kwa wao kuosonga mbele pia.

3. Unaacha historia
Unaposonga mbele huku unapopita unaacha historia na somo kwa vizazi vijavyo vitajifunza mengi kwa yale uliyo yafanya na kuyaacha duniani. Jiulize umejitahidi sana umepata mafanikio makubwa hapa duniani lakini ukafanya uzembe kidogo ukapoteza vyote ulivyovipata, Unafikiri utakumbukwa kwa lipi zaidi? Watasema alikua tajiri lakini mali zake zilipotea ghafla, au alipokua muimbaji alikua maarufu sana alipolewa umaarufu ndipo akapotea,

Unapofikia mwisho mzuri unaacha historia nzuri, maisha ni sawa na safari ya basi, tunasafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, gari inapopata pancha hakuna abiria anaefurahia wote wanatamani safari iendelee, Gari linaposimama watu kujipatia chakula haina maana ni mwisho wa safari hivyo mfanikio uliyoyapata sasa yasikufanye ubweteke gari bado linasonga na mwisho wa safari hii ya maisha ni kifo peke yake hivyo tuendelee kusonga mbele .

Asante sana na Karibu
©Jacob Mushi 2016
Tuandikie 0654726668 E-mail jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading