Kitabu hiki nimeandika kwa ajili yako. Kuna mambo mengi sana ya kujifunza ndani ya kitabu hiki na nina imani kitakua ni sababu ya wewe kusogea katika eneo lile ulilokua na kwenda mbele Zaidi.
Utajifunza, Jinsi ya Kujua Kusudi Lako, Siri na Sababu za Kuwepo Hapa Duniani, Kugusa maisha ya wengine, Kufikia Ukuu, Kufika kilele cha Mafanikio, Kuishi maisha bora, Kutengeneza Na Mungu Wako, Kutambua kile Mungu ameweka ndani yako, Kufikia Ushindi Mkubwa.
Watu wengi wanaishi Maisha ambayo hayana mwelekeo, wanafanya kazi wasizozipenda, wanaishi Maisha wasiyoyataka kwa maana kuwa hayawapi furaha. Hii yote inaletwa na kutokujua sababu hasa ya wao kuwepo hapa duniani. Kitabu hiki kitakwenda kukufungua macho.
Utajifunza:
- Kusudi la Wewe Kuwa Hai.
Ili uweze kuishi Maisha yenye mwelekeo mzuri na kujua ni kipi hasa unapaswa kufanya kila siku ni hadi utakapoweza kutambua kusudi la wewe kuwepo hapa duniani. Kitabu hiki kimeeleza namna yaw ewe kugundua kusudi lako.
- Kugusa Maisha ya Wengine.
Kila unachokifanya hapa duniani kinaongezeka sana endapo kitakuwa kinagusa Maisha ya wengine. Kiwango cha Maisha uliyogusa ndio kiwango cha mafanikio yako.
- Kutengeneza Historia Mpya.
Ni alama gani unataka kuacha hapa duniani? Haijalishi umeshafanya makosa mangapi kuwepo kwako leo kunakupa nafasi ya kutengeneza historia mpya. Kitabu hiki kitakupa mwongozo huo.
- Kuishi Maisha ya Ushindi.
Unatakiwa uishi Maisha ya ushindi kila siku kwenye kila unalolifanya. Utajifunza mbinu za kupata ushindi kwenye kila unachokigusa na mikono yako.
Reviews
There are no reviews yet.