508; Atawainua Kunguru Wakulishe.

1 Wafalme 17:4,6 [4] Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko. 6. Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito.

Nimewatafakari wale Kunguru waliomlisha Elia nyama na mkate tena kipindi ambacho nchi ilikuwa imekosa mvua karibu miaka mitatu (maana yake kulikuwa na njaa) nikagundua Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote ili amsaidie yule anaemtaka. Kuna watu huwezi kuwaamini kwasababu ya tabia zao lakini kuna nyakati Mungu atawatumia wakusaidie. Kama kunguru alibeba pande la nyama na hakuthubutu kulionja akampelekea Elia basi hata watu wauaji wanaweza kukuokoa wewe wakati maadui zako wanataka kukumaliza. Mungu anaweza kumuinua kibaka akusaidie upite salama kwenye njia yenye vibaka.

Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote anapotaka kusudi lake litimie. Usiwaze sana hasa pale unapojiona uko mwenyewe, hakuna anaekutazama, hakuna anaeulizia hali yako. Yote hayo Mungu anaweza kuyatatua kwa kumgusa mtu yeyote atamkaye aje awe upande wako.

Usimkatie Tamaa Mungu, usione kachelewa, usiseme hakuoni, endelea kumuamini na kumtumainia kila wakati.

Usiishie Njiani.

Rafiki yako

Jacob Mushi.

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading