Wanadamu wana tabia ya kuongea bila kufahamu na ukifanya makossa ukawasikiliza wanaweza kukupoteza. Tukimtazama kijana Daudi aliekuwa mchunga kondoo porini, baba yake na ndugu zake walimchukulia kama mchunga kondoo, na kijana mdogo tu. Lakini Mungu mwenyewe alikuwa ameshamchagua kuwa mfalme wa Israel.
Kwa akili za kibinadamu mara zote tunatazama nje. Watu wakikutazama kwa nje wanaona huna uwezo wowote lakini ndani yako Mungu ameweka uwezo mkubwa sana ambao hauonekani kwa macho ya kawaida.
Nataka nikwambie kwamba sikiliza kile ambacho Mungu anasema juu ya Maisha yako. Achana na maneno ya watu kwasababu yatakuyumbisha na kukufanya uanze kujiona hufai na huwezi tena kuitimiza ndoto zako.
Unamsikilizaje Mungu? Kwa kupitia neno lake, jijengee tabia ya kulisoma neno la Mung una utaweza kuisikia sauti ya Mungu ikinena katika Maisha yako. Unapopitia nyakati ngumu Usiishie tu kulalamika na kusema Mungu hakuoni chukua muda wako usome maneno ya Mung una utaisikia sauti ya Mungu ikinena nawe.
Ukiwasikiliza wanadamu utapotea kwasababu hawana uwezo wa kuona vile Mungu anaona. Wengi watakueleza kile ambacho macho yao yanaona.
Nakutakia Kila la Kheri.
Rafiki Yako Jacob Mushi