Hello Rafiki yangu, leo ni siku ya kumi yam waka 2020 siku zinaendelea kukatika bado kidogo tutasikia mwaka upo nusu. Je bado waendelea kusubiria kidogo ndio uanze kufanya mambo yako? Rafiki yangu utachelewa sana kama hutakuwa mtu wa tofauti.

Mwaka mpya bila ya akili mpya mtazamo mpya, hakuna kitakachobadilika. Aya ngoja niachane na hayo usije ukajisikia vibaya ukaacha kusoma.

Leo nimekuandalia Makal kuhusu sehemu 3 za Muhimu sana kuwekeza kwenye Maisha yako kila siku. Hizi ni sehemu ambazo inawezekana hujawahi kufahamu kwamba uwekezaji unahitajika. Watu wengi wakisikia uwekezaji hufikiria Zaidi mambo ya fedha, hisa, mashamba, majengo n.k. lakini kumbe kuna sehemu nyingine. Kwenye Makala hii utakwenda kuziona vizuri.

Jana nimeandika Makala inahusu kuwekeza Tsh 40,000/= (elfu arobaini) halafu ikurudishie tsh 400,000/= ndani yam waka mmoja (Unaweza kuisoma kwa kubonyeza maneno haya.). kuna watu waliisoma na hawakuelewa vizuri sasa kwa kupitia Makala hii ya leo utaweza kufahamu vizuri Zaidi.

Ukweli uwekezaji Upo sehemu Zaidi ya moja na watu wenye mafanikio hupenda kutuambia kwamba tuwekeze Zaidi kwenye akili zetu, maana yake kuwekeza kwenye akili ni sehemu nyingine pia ya kuwekeza. Wewe unavyosoma Makala hii kujifunza unawekeza pia, kuna vitu utavifahamu vitakusaidia leo au miaka kumi ijayo. Uwezo wa kusoma ulionao hukujua leo uliwekeza kwenye elimu na sasa kwa kupitia elimu unaweza kuvuna matunda sasa hivi.

Sasa nisikuchoshe twende kwenye hizo sehemu tatu muhimu sana kwenye Maisha yako kuwekeza kila siku.

a/ Uwekezaji kwa Kupitia Kipato/Mali.

Hapa tunazungumzia uwekezaji unaotokana fedha au mali ambazo mtu anamiliki. Wewe unalipwa mshahara wa milioni mbili kwa mwezi basi ukaamua uwe unawekeza Tsh laki tano katika ule mshahara wako kwenye uwekezaji wa aina mbalimbali mfano ukanunua HISA, ukanunua mashamba, ukaanza ujenzi wa nyumba za kupangisha n.k. huu uwekezaji umezoeleka sana na mtu anaposikia kuhusu uwekezaji anaelewa moja kwa moja ni mambo haya.

b/ Uwekezaji Ndani yako.

Hapa sasa tunaingia kwako wewe binafsi, tunagusia AFYA, AKILI, NA ROHO YAKO. Ukisikia mtu ana matatizo ya presha au kisukari au uzito ulipitiliza mara nyingi sababu zinakuwa huyu mtu alishindwa kuwekeza kwenye afya yake. Alishindwa kuupa mwili vyakula vyenye afya kwa ajili ya Maisha ya baadae. Sasa kuwekeza kwenye afya ni kutengeneza afya bora ambayo itakuwezesha wewe uweze kuishi vizuri miaka 10,20, 50 ijayo.

Kuwekeza kwenye akili yako ni kuhakikisha unajilisha maarifa ya kutosha ili uweze kuleta mabadiliko kwenye Maisha yako baadae. Kuna vitu unaweza kujifunza leo vikabaki vinakuingizia faida Maisha yako yote yaliyobakia.  

Pia Kuwekeza kwenye Roho hapa ni kujenga mahusiano bora kati yako na Mungu. Najua unaamini Mungu yupo. Sasa kama hutawekeza kwake unafikiri mwisho wako utakuja kuwaje? Siku ukiondoka utakwenda kumwambia nini?

Yule mtu ambaye unataka kuwa hatokei tu kiarahisi inahitajika nguvu kubwa katika kuwekeza ndani yako. Lazima uhakishe unakuwa na AFYA BORA, MAARIFA NA HEKIMA hivi vitakusaidia kuwa mtu bora ambaye ana mchango mkubwa kwenye Maisha yako na wengine.

c/ Uwekezaji kwa Wale Uwapendao/Ndugu/Marafiki na Jamii.

Huu ni uwekezaji kwa wale unaowapenda na kwa jamii inayokuzunguka. Hapa kwa wewe ambaye una mke/mume/Watoto/ndugu na marafiki utapaswa kufanya kitu kwa ajili yao.

Vile vile utapaswa kufanya kitu kwenye jamii inayokuzunguka. Sio lazima ukifanyacho kiwe ni kinahitaji fedha bali kiwe ni kitu chenye kuongeza thamani na kinachogusa Maisha yao. (Jamii inaweza Kuwa Mtaa Unaoishi/ulikotoka, kanisani/msikitini unakosali.).

Kwa kupitia kuwekeza kwa hawa watu miaka ijayo utakuja kuyaona matunda ya uwekezaji wako. Utazungukwa na jamii ambayo inatokana na uwekezaji wako kwao. Utaishi Maisha ya furaha kwasababu uliweza kuitengeneza jamii ambayo ulikuwa unaitaka.

Mke/mume/Watoto hawawezi kuwa vile unavyotaka kama wewe hujachangia. Badilisha kile unachowekeza kwao kila siku. Maneno yako unayoongea nao ni uwekezaji, vile unavyowatendea ni uwekezaji miaka michache ijayo watakuwa kile ulichokuwa unawafanyia.

Sasa jiulize wewe umepambana tu kuwekeza kwenye fedha ukaisahau jamii, kukaibuka kizazi cha watu katili sana. Hawa watu watakuja kukudhuru wewe au wale unaowapenda. Lakini ukiwekeza japo kwa kuwaonesha upendo na kuwajali utajiepusha na madhara.

Haya Rafiki tayari nimegusia sehemu tatu za Muhimu kuwekeza kwenye Maisha yako kila siku. Nimeadnaa Program inaitwa WEKEZA CHALLENGE 2020 ambayo tutakuwa tunayalenga maeneo haya matatu kwa mwaka huu 2020 na kuendelea. Itakuwa vyema sana ukijiunga kwasababu itakusaidia kuwa mtu bora sana.

Ili kujiunga na program hii yakupasa kulipa ada ambayo ni Tsh 40,000/= kwa mwaka mzima. Kujiunga Unaweza kulipa ada moja kwa moja kwenye namba za Tigopesa 0654 726 668 au Mpesa 0755 192 418 majina yanatokea Jacob Moshi. Baada ya kulipia Nitumia ujumbe kwenye WhatsApp namba 0654 726 668 wenye majina yako na neno WEKEZA.

Karibu Sana

Rafiki Yako

Jacob Mushi.

5 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading