Mojawapo ya sehemu ambayo utakosea ni kusahau sehemu hizi nne za muhimu kwenye maisha yako ambazo unatakiwa uwe bora kila siku. Unajua ili uweze kuwa na mwili mchangamfu na wenye afya hutakiwi kula chakula kizuri pekee yake, lazima utatakiwa uwe unaufanyia usafi mwili, pia ufanye na mazoezi. Kama utakula peke yake ukasahau kuufanyia usafi mwili utanuka. Kama utakula vizuri na utaufanyia usafi mwili bila ya kufanya mazoezi utajitengenezea mwili mbaya.

Hivyo ni muhimu sana kujua kila sehemu ina umuhimu wake kwenye mwili wako na unapaswa kufanyia kazi. Vilevile kwenye maisha unapaswa kujua sehemu za muhimu sana ambazo ukikosea mojawapo huwezi kuishi maisha yenye furaha.

Tengeneza Afya Bora.

Msingi wa muhimu na wa kwanza katika maisha ya mafanikio ni afya yako. Ili uweze kufanya vitu vingine vyote huku duniani kwanza lazima uwe na afya bora. Kama una afya mgogoro ufanisi wako katika kazi utapungua.

Ni muhimu sana kuhakikisha unakuwa na afya bora ili uweze kuwa na uzalishaji mzuri kwenye kila sekta ya maisha yako. Kama una afya mbovu huwezi kufurahia mahusiano, huwezi kufurahia pesa ulizonazo pia hata kuzitafuta hutaweza vyema.

Ili kuwa na afya bora hakikisha unakula vyakula bora hasa vyakula vya asili. Kipindi hiki vyakula vingi havipo salama. Hivyo ni bora kula vyakula kutoka ardhini Zaidi kuliko vya madukani na viwandani.

Usijidanganye kula vizuri ni hadi uwe na pesa nyingi, vyakula vingi vya asili bei zake ni za kawaida kabisa kama ambavyo unachotakiwa ni kaucha vyakula vyenye mafuta mengi sana na vya kukaanga. Pia jaribu kuufata ushauri wa wataalamu wa afya juu ya vyakula unavyopaswa kutumia.

Hakikisha unafanya mazoezi mara kwa mara, ikiwezekana kila siku. Hii itaufanya mwili wako kuondoa sumu za aina mbalimbali zinazoukabili. Mazoezi yatakufanya uwe na uwezo mzuri wa kufikiri ukiwa kwenye shughuli nyingine.

Hakikisha unakuwa na utaratibu wa kucheki afya yako mara kwa mara ili kujua mwili wako uko kwenye hali gani.

Mahusiano Bora.

Kwenye hii dunia kama utakula vizuri na utaweza kupata kipato chochote unachokitaka ukakosea kwenye mahusiano bado unaweza kukonda kama watu ambao wana shida ya chakula. Ukitaka kuvuruga maisha yako ni pale utakapofanya makossa kwenye mahusiano ambayo umechagua.

Mahusiano haya ninazungumzia kwa upana wake kuanzia marafiki unaombatana nao, mpenzi wako, na jinsi unavyokaa na jamii inayokuzunguka. Ili uweze kuishi vizuri na kwa furaha lazima uchague marafiki wazuri ambao wanafanana na wewe. Wana ndoto kubwa kama zako.

Lazima uchague mwenza sahihi kulingana na maono yako. Sio mtu alievutiwa na uzuri wako au alievutiwa na pesa zako bali anaendana na kule unapotaka kwenda.

Ni muhimu uwe mtu unaejali wengine hasa jamii inayokuzunguka. Kwa kupitia vitu ambavyo Mungu ameweka ndani yako unapaswa kuvitoa nje kwa watu wafaidike navyo.

Fanya kile Unachokipenda.

Kama utafanya kitu kwasababu tu unapata pesa huwezi kukifanya kwa ufanisi mkubwa. Huwezi kuwaza mbali sana juu ya kitu kile sana utawaza pale mahitaji yako ya kifedha yanapoishia peke yake.

Lakini unapofanya jambo kwasababu ni kitu kutoka ndani yako siku zote utakifurahia sana. Maisha yako yote na nguvu zako zote unaweza kuziweka kwenye kile unachokipenda ili ufikie mafanikio makubwa. Unapofanya unachokipenda unakuwa na hamasa kubwa Zaidi kuliko kufanya kile kinachokulipa pesa nzuri pekee yake.

Unaweza kufanya kazi inayokupa msongo wa mawazo na maumivu ya kicha kwasababu tu huipendi kazi yako. Unaweza kuwa mtu ambaye unachukia sana inapokuwa asubuhi na kufurahi inapokuwa jioni kwasababu ya kazi yako huipendi.

Ni nyema sasa uanze safari hapo ulipo sasa kuelekea kwenye kufanya kile unachokipenda. Hakuna njia nyingine ambayo utaweza kufanya kwa kujitoa sana na bidi kubwa kama hupendi unachokifanya.

Matokeo mazuri kwenye kazi yanasababishwa na msukumo kutoka ndani na sio kutoka nje.

Tengeneza Kipato Cha Kutosha.

Ukiweza kuwa na afya bora, ukafanikiwa kujenga mahusiano bora na ukaweza kufanya unachokipenda unapaswa kujua kutengeneza kipato cha kutosheleza mahitaji yako ya kila siku na ya baadae.

Kwa kupitia kazi yako unapaswa kujua namna gani bora ya kutengeneza kipato cha kutosheleza mahitaji yako.

Unapaswa kujifunza tabia na kanuni za utajiri. Ili uweze kufurahia maisha katika viwango vya hali ya juu unapaswa kuwa tajiri. Ili kuboresha mahusiano yako Zaidi, afya yako na akili yako pia unapaswa kuwa na kipato cha uhakika na cha kutosha.

Mojawapo ya sababu zinazoleta msongo wa mawazo ni watu kutokujua kuhusu kesho yao. Kipato kutotosheleza mahitaji. Hivyo basi ili uweze kuwa na akili bora, uwezo mzuri wa kufikiri jifunze namna ya kutengeneza kipato cha kutosheleza mahitaji yako.

Kuna aina ya maisha huwezi kuyaishi kabisa kama huna uhuru wa kipato. Kama unataka kusafiri, kuendesha gari unalopenda, kuishi kwenye nyumba unayotaka, na kuwasaidia wengine kifehda, huwezi bila ya kuwa na uhuru wa kipato. Ukikosea ukajilazimisha utaishia kwenye madeni makubwa. Anza kwanza kutengeneza uhuru wa kipato

Ni muhimu sana ukazingatia haya katika maisha yako kila siku ili uweze kufurahia maisha. Haijalishi uko wapi sasa hivi bado una nafasi ya kutengeneza upya. Unaweza kujenga upya afya yako, mahusiano yako, unaweza kuanza kufanya kile unachokipenda sasa hivi na pia una nafasi ya kutengeneza uhuru wa kipato bila ya kujali umri ulionao.

Rafiki Yako,

Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading