Kila serikali huendeshwa kwa sheria na taratibu mbalimbali ambazo huwezesha watu kuishi kwa pamoja na kupunguza matatizo mbalimbali.

Nimejiuliza kama mpaka sasa kungekuwa hakuna serikali, wala mipaka ya nchi yaani mtu peke yake anaibuka tu anafanya kila anachotaka tungekuwa wapi? Ukweli ni kwamba kuna vingi tungekosa na kuna vingi vingepotea.

Sasa kama ni hivyo wewe binafsi unapaswa kuwa na sheria, kanuni, taratibu za maisha yako ambazo zinaweza hata zisifanane na mtu mwingine. Na wakati huo huo lazima pia uangalie sheria hizi zisiwe zinayabughudhi maisha ya wengine.

Ili uweze kufikia mafanikio makubwa lazima uweze kujiongoza, kujidhibiti, kujifanyia maamuzi sahihi. Kinachowafanya watu wengi wanafeli ni kukosa kujidhibiti binafsi.

Lazima ujiwekee sheria zako mwenyewe ambazo utakuwa unazifuata popote pale kwenye maisha yako. Mfano mimi hapa nina sheria zangu kadhaa ambazo huwa nazifuata.

Sasa zipo nyingi sitaweza kukutajia hapa mengine ni mambo ya siri, wewe huo ni mfano unaweza kuutumia katika yale mambo ambayo unaona yamekuwa kama ni mzigo kwako katika kukurudisha nyuma.

Tengeneza Sheria na taratibu ambazo utazifuata siku zote za maisha yako bila kujali upo wapi. Ukisema situmii vinywaji vyenye sukari simamia tu bila kujali umeenda wapi na upo na nani.

Ukijiwekea utaratibu kwamba wewe hutumii chakula mchana nenda na utaratibu huo hata kama upo kwa wakwe zako, (hahaha natania).

Maisha yako hayataweza kusimama kama huna utaratibu ambao unaufuata kila siku na kuuheshimu sana.

Ili kutengeneza tabia kama hizi ambazo zitakuwa na mchango mkubwa kwenye mafanikio yako utapaswa pia kuwa na mtu wa kukusimamia sio siku moja kama vile umekunywa dawa lazima itachukua muda hadi uzoee.

Kama utahitaji niwe nakusimamia kwenye kutengeneza Sheria, taratibu na kanuni za maisha kama hizi Usisite kuwasiliana nami.

Kupata huduma mbalimbali ninazotoa tembelea kwenye link hii www.jacobmushi.com/huduma

Nakutakia kila Kheri

Rafiki Yako

Kocha Jacob Mushi.

2 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading