Shukuru kwa uhai ulionao leo kwani kuna wengine hawajaamka.

Shukuru kwa macho ulionayo na yana uwezo mzuri wa kusoma na hata leo umeweza kusoma makala hii. Wako wengine ni vipofu na hawana uwezo kama wako.

Shukuru kwa nguvu za kuweza kusoma jumbe hizi kuna wengine ni wagonjwa hata simu hawawezi kushika.

Shukuru kwa watu wazuri Mungu aliokupa wanakujali na kukusaidia kwani kuna wengine hawana ndugu hawana watu wa karibu hawana mtu wa kumuelezea shida zao wamebaki peke yao duniani.

Shukuru kwa kuzaliwa kwenye nchi yenye amani unaweza kufanya mambo mengi mno bila kuzuiwa na chochote wako waliozaliwa vitani maisha yao yote ni kukimbia.

Shukuru kwa elimu uliyonayo kuna ambao wanatafuta namna waende shule na hawajapata hawajui wafanye nini.

Shukuru kwa kuweza kupata chakula cha leo hujalala njaa kama wengine wako ambao chakula ni tatizo kubwa sana Ukiweza kuwatatulia shida yao ya chakula unakua umewasaidia sana.

Shukuru kwa vipaji, fursa, uwezo mzuri wa kufikiri, na watu wengi wa kipekee ulionao kwenye maisha yako wanafanya maisha yako yawe bora wengine hawana ulichonacho wewe.

Shukuru hata kwa simu nzuri ya kisasa au computer uliyonayo inakuwesha kusoma makala hizi kila siku kuna wengine hawana kwa hiyo maarifa haya hawayapati.

Shukuru kwa ufahamu ulio nao kuna wengine hawana na hawajui wafanye nini.

Upo kwenye nafasi Nzuri ya kufanikiwa sana kama utaweza kuona mambo mengi uliyonayo na wengine hawana. Una mengi ya kumshukuri Mungu.

Uzue ulimi na fikra zako kulalamika angalia vitu ulivyonavyo na ni wangapi wanavitafuta na wakipewa maisha yao watayaona ni bora.

Leo ni wakati wako wa Kushukuru.
Haupo hai kwa bahati mbaya.
Upo Hai Kwa Kusudi.

Karibu sana.
Mushi Jacob

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading