Habari za Leo Rafiki na Mwanamafanikio mwenzangu. Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vyema na afya pamoja na safari hii ya mafanikio. Siku zote napenda kukwambia kamwe usikate tamaa. Haijalishi ni magumu kiasi gani unapitia sasa. Ipo siku Matokeo ya unachokifanya yatakuja kuonekana.

Leo tujifunze juu ya Sifa tano ambazo zinaonyesha mtu huyu anaelekea Kwenye Mafanikio Makubwa.  Zipo sifa nyingi lakini mimi nimechagua 5.

  1. Mwanafunzi

Mtu yeyote ambaye anaelekea au tayari ameshaanza kuyaona mafanikio makubwa hua ana sifa ya uanafunzi. Sifa hii iko kwake kwasababu anajifunza kila siku Kwenye vitu anavyofanya, anavyopishana navyo,  kwa wengine,  kusoma vitabu,  na mabadiliko ya kiteknolojia ili kuboresha yale anayoyafanyia kazi.

Kama wewe unataka kuwa na mafanikio makubwa kamwe usithubutu kuhitimu kujifunza.  Usifike mahali ukasema mimi tayari ninajua kila kitu, au tayari nina kipato cha kutosha najifunza ya nini? Hata kama umeshapata kila unachokitaka kumbuka pia unaweza kupoteza vyote muda wowote. Hata kama wewe umeshakua milionea tambua unatakiwa ujifunze ili uwe bora zaidi watu wasikuchoke au kuzoea kile unachokitoa.

SOMA : HII NDIO TABIA ITAKAYOKUFANYA UWE MASIKINI SIKU ZOTE.

  1. Mtendaji

Sifa ya pili ni ya utendaji.  Mtu yeyote anaelekea au mwenye mafanikio makubwa siku zote hua ni mtu wa vitendo.  Akijifunza kitu kipya lazima akiingize kwenye vitendo. Amekutana na wazo jipya lazima alifanyie kazi. Hivyo sifa hii humfanya aendelee kuyaona mafanikio kila wakati kwenye yale anayoyafanya.

 

Katika programu tulizonazo kwenye simu zetu mara nyingi hua zinatuambia *Update*. Maana yake ni nini sasa ni kwamba kutokana na wateja au watumiajivwa programu hizi kutoa malalamiko au kushindwa kutumia vyema programu hizi wamiliki wake wanaongezea vitu bora zaidi ili kumrahisishia mtumiaji.  Na hili linawafanya watumiaji kufurahia zaidi vile vitu vipya. Je na wewe hua unafanya *mabadiliko* kwenye biashara zako?  Huduma unazotoa?  Lazima uweke kwenye vitendo vile unavyojifunza,  malalamiko ya wateja na ulete mabadiliko haijalishi tayari umeshakusanya watu wangapi wanaweza kuhama wote.

 

  1. Mtu wa Shukrani.

Sifa nyingine na ya muhimu sana ni Shukrani. Mtu mwenye mafanikio makubwa au anaeelekea huko hua anashukuru kwa kila analopitia,  kila hatua anayopiga hua anashukuru.

Kinyume cha mtu ambaye hana Shukrani ni yule ambaye analalamika na kulaumu. Kama wewe siku zote hua unaona lawamabtu huoni kitu cha kushukuru upo kwenye hatari ya kurudi nyuma kabisa.  Anza leo kuhesabu mambo ya kushukuru na acha kabisa lawama. Yapo mengi sana ya kusema asante mbele za Mungu wetu kila kukicha. Nafasi ya kuwepo tu duniani siyo ya bure ni ya pekee sana, unapaswa kusema asante hata kwa hiyo.

Shukuru kwa mali ulizonazo ni kwa kusudi la Mungu uzimiliki wewe na sio mwingine. Sio bidii zako pekee bali na Mungu ameruhusu. Mungu ametoa kibali kwa watu na wakapokea kile unachokifanya.

Kila ifikapo Asubuhi mpya shukuru Mungu,  iwapo Jioni Shukuru Mungu.

 

  1. Mtoaji.

Kama ulikua hujui hii ni sifa ambayo inawafanya waliofanikiwa waendelee kupata mafanikio zaidi.  Utoaji ni chanzo cha mafanikio yote. Kama wewe utafikiri labda wenye mafanikio ni wachungu jaribu kuwachunguza.  Ni watoaji wazuri sana,  na wanafanya hivyo siku zote.

Kama wewe unafikiri huwezi kutoa kwasababu huna basi ujue hutakaa upate cha kutoa. Wako waliotoa hadi watoto ili wawe sadaka mbele za Mungu. Sisemi ukatoe watoto bali nataka kukuonyesha jinsi ambavyo ulivyo na vingi vya kutoa. Unaweza kutoa muda wako pia hata kama huna pesa. Toa muda wako kuwasaidia wengine. Mungu atarudisha maradufu yale uliyoyatoa.

Usitoe ili ujulikane umetoa hakikisha ni wewe pekee umejua pamoja na Mungu wako. Biblia inasema hata mkono wako wa pili usijue ni kitu gani mkono wako mwingine umetoa.  Yaani hata jirani yako wakati mwingine asijue ni nini umetoa.

Wakati mwingine hata mwenzi wako asijue ni ninj unataka kutoa kwani anaweza kuwa sababu ya wewe kutokutoa.  Nadhani mnakumbuka Anania na Safira.  Kuna vitu ambavyo unajua kabisa hivi nikisema sitapata kibali hivyo najitoa muhanga tu.

Toa! Toa! Toa!  Utapokea bila kujua.

 

SOMA : JINSI YA KUEPUKA MADENI MABAYA NA KUFIKIA UHURU WA KIFEDHA

 

  1. Mwenye Upendo

Haiwezekani wewe ukawa na maono makubwa halafu unapoteza muda kujenga chuki na watu wengine. Haina maana kabisa wewe uchukiane na tajiri mwenzako kwasababu tu anakupita katika mauzo. Leo nikwambie upendo ndio kila kitu kwenye Dunia ya sasa. Bila upendo ni kazi bure yale tuyafanyayo. Upendo ndio chanzo cha mema yote duniani. Anza leo kusamehe, Ondoa vinyongo na wengine, sahau kila kitu kibaya ulichotendewa angalia uzuri wa Bwana. Watu wenye mafanikio wanawapenda wengine pamoja na wenyewe kwa wenyewe. Mshindani wako wa Kibiashara sio adui yako.

Karibu sana.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

“Piga Hatua”

One Response

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading