Mojawapo ya changamoto kubwa wanayopitia wengi sana ni kukosa timu ambayo inaweza kuwa sababu ya wao kufikia mafanikio makubwa.

Kuna usemi unasema kama ndoto zako, maono yako utaweza kuyatimiza wewe peke yako basi hayo sio maono ya kutoka kwa Mungu. Vilevile kama utaweza kufanya wewe kila kitu na ndoto zikatimia basi hizo ndoto ni ndogo sana.

Mungu akikupa maono sio kwa ajili yako ni kwa ajili ya wengi. Hivyo utahitaji watu ambao watakuwa msaada kwako kwa vitu vile ambavyo hutaweza kuvifanya au ulivyopungukiwa.

Karibu manabii wote wakubwa ambao tumewasoma kwenye vitabu vya Mungu walikuwa na wajakazi wao ambao baadae nao walikuja kuwa manabii tena. Kuna vitu hutaweza kuvitekeleza peke yako.

Ukishaanza kuona dalili ya kuzidiwa majukumu anza kuandaa watu ambao wataweza kwenda pamoja na wewe ili kutimiza yale maono makubwa ndani yako. Vilevile kile unachokianzisha utakiacha hapa duniani hivyo wale uliowaandaa watakuwa wabeba maono yako na kuyaendeleza hapa duniani hata kwa vizazi vingine.

Nimekuandalia sifa chache ambazo unaweza kuziangalia kama za kwanza kabisa wakati unataka kuchagua watu ambao watakuwa ni timu yako ya mafanikio.

Kigezo hiki nimekiweka cha kwanza kabisa kwasababu hata akiwa na sifa nyingine zote lakini akashindwa kuwa tayari kwa yale  maono yako kazi yake haitakuwa na maana yeyote. Tuna mwona Yesu wakati anakusanya wanafunzi alipofika kwa wakina Petro wakivua samaki aliwaambia waache kuvua samaki atawapeleka wakavue watu. Sasa hapa tunaona ni namna gani hawa waliona kile wanachokifuata ni kikubwa kuliko wanachokifanya kwa wakati ule.

Kama mtu hayuko tayari hakuna haja ya kwenda nae atakusumbua njiani. Lazima kwanza awe tayari kukufuata hata kabla hajapata maslahi yeyote.

Sifa ya pili ni muhimu sana wawe ni watu wanaoamini katika kile unachokiamini wewe. Sizungumzii Imani ya kidini bali nazungumzia Imani katika misingi ya mafanikio.

Ukiwa na watu wanaoamini kushindwa, wanaamini waliofanikiwa ni wachawi, wameiba, mafisadi watu hawa watakutesa mno. Hawataamini hata wewe kuwa ni msafi.

Hakikisha sana unakuwa na watu wanaomini katika kufanya kazi kwa bidii, kujitoa, uadilifu na kujituma.

Tafuta watu ambao wanakuja kuziba yale mapungufu yako. Kama kuna sehemu ambazo unajua wewe hauko vizuri basi usikosee ukaleta watu tofauti.

Hii itakuwezesha wewe uweze kuwa na matokeo bora kila wakati. Kwenye timu ya mpira kila namba ina kazi yake na majukumu yake pia.

Namba tisa hawezi kufanya kazi ya kipa uwanjani hakutakalika. Kipa yeye kazi yake ni kudaka. Kama kocha akileta watu ambao ni wazuri kwenye kudaka mpira tu kisha akawapangia namba mpira utakuwa ni mgumu sana.

Hivyo pia katika kuchagua watu usije kuchagua watu ambao ujuzi wako na wao unafanana. Tafuta watu ambao wanakuja kuziba mapungufu yako.

Soma: Siri Iliyopo Ndani ya Woga.

Ni muhimu sana ukatafuta watu ambao ni waadilifu kwasababu hawa ndio watajenga sifa nzuri ya kile unachokifanya. Ukileta watu wenye tamaa, wezi, wasiojua kuheshimu watu mwisho wa siku na wewe utaonekana unafanana nao.

Hakikisha watu ambao unafanya nao kazi wanakutambulisha vile unavyotaka kutambulika. Wanazungumza kile ambacho unatamani watu wakisikie.

Watu wenye tamaa wanaweza kuja kuwa sababu ya wewe kupoteza sifa bora ya kile unachokifanya.

Sifa ya mwisho ni watu ambao wanafanya kazi kwa bidii. Kama utachukuwa watu wavivu watakuwa wanakuangusha kila wakati.

Pale unapotaka jambo Fulani liwe tayari wanaweza kuwa sababu ya kukuzungusha na kuzungusha wateja wako.

Kama utakosea na ukaleta watu wajanja wajanja watakuharibia kazi na mwishoe utaonekana wewe hauna ubora katika kazi zako.

Mafanikio na ushindi yanaletwa na timu bora. Hakikisha timu yako haina watu wabinafsi ambao wanafanya ili waonekane wao, bali kuwa na watu ambao wanafanya kwa ajili ya timu na kwa ajili ya maono yako.

Ukichagua vyema Timu yako Mafanikio ni Lazima.

 

”Kama umependa Makala Hii Usiache Kuweka Maoni yako Hapa chini”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

 

Jacob Mushi,

Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,

Simu: 0654 726 668,

Instagram: jacobmushi

Facebook: Jacob Mushi Page                                                                   

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com 

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading