Connect with us

SIKU MPYA, AKILI MPYA, NGUVU MPYA.

MAISHA NA MAHUSIANO

SIKU MPYA, AKILI MPYA, NGUVU MPYA.

Habari Rafiki, Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi. Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote. “NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA. MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE. Mungu alijua kabisa Musa angekulia katika familia yake angekuzwa na mtazamo […]

Habari Rafiki, Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi.

Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.

“NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA.
MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE.

Mungu alijua kabisa Musa angekulia katika familia yake angekuzwa na mtazamo wa kitumwa, akamtoa akampeleka kwa mfalme ili akuzwe kwa mtazamo wa kifalme. Wakati mwingine inakupasa uondoke sehemu uliyoizoea ili ukajenge mtazamo mpya wa kukuwezesha Kutimiza Ndoto zako.

Wana wa Israeli walipokuwa Jangwani wakapitia shida kidogo ya njaa Wakaanza kukumbuka vyakula vizuri walivyo kuwa wanakula Misri.

Walisahau kabisa kwamba Misri hapakuwa kwao, walipitia mateso, walitengeneza tofali, Farao aliua watoto wao wote wa kiume. Haya yote hawakukumbuka wao walikumbuka chakula tu.

Wewe changamoto unazopitia kwenye Safari ya mafanikio zisikufanye uanze kukumbuka maisha fulani ya nyuma, kipindi ukiwa umeajiriwa, kipindi ukiwa na mpenzi wako wa zamani, kipindi upo na wazazi wako, na mengine mengi.

Lolote linalotokea mbele yako Pambana nalo uhakikishe unavuka.

Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana,
Rafiki Yako, Jacob Mushi

Continue Reading
You may also like...

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in MAISHA NA MAHUSIANO

To Top