Habari Rafiki, Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi.

Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.

“NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA.
MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE.

Mungu alijua kabisa Musa angekulia katika familia yake angekuzwa na mtazamo wa kitumwa, akamtoa akampeleka kwa mfalme ili akuzwe kwa mtazamo wa kifalme. Wakati mwingine inakupasa uondoke sehemu uliyoizoea ili ukajenge mtazamo mpya wa kukuwezesha Kutimiza Ndoto zako.

Wana wa Israeli walipokuwa Jangwani wakapitia shida kidogo ya njaa Wakaanza kukumbuka vyakula vizuri walivyo kuwa wanakula Misri.

Walisahau kabisa kwamba Misri hapakuwa kwao, walipitia mateso, walitengeneza tofali, Farao aliua watoto wao wote wa kiume. Haya yote hawakukumbuka wao walikumbuka chakula tu.

Wewe changamoto unazopitia kwenye Safari ya mafanikio zisikufanye uanze kukumbuka maisha fulani ya nyuma, kipindi ukiwa umeajiriwa, kipindi ukiwa na mpenzi wako wa zamani, kipindi upo na wazazi wako, na mengine mengi.

Lolote linalotokea mbele yako Pambana nalo uhakikishe unavuka.

Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana,
Rafiki Yako, Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading