Muda ndio maisha yetu maana ndio thamani ya pekee tuliyonayo kuliko chochote. Unapompa mtu muda wako unakua umempa kitu cha thamani sana kuliko kitu chochote kile. Unakua umemgawia sehemu ya maisha yako. Watu wengi wanashindwa kuthamini muda kwasababu hawajajua thamani yake. Mtu anapotenga muda kwa ajili yako ni sawa na ametoa sehemu ya maisha yake akakupa au akaa na wewe. Hatujui tutaishi kwa muda gani huku duniani lakini kila mmoja ana muda wako wa kuwepo duniani. Kama kuna zawadi ya maana sana ya kumpa mtu ni muda wako. Kwenye maisha yetu ya sasa wengi wanajali Zaidi vitu kuliko muda. Mtu anajali pesa kuliko muda. Lakini muda ndio unaleta kila kitu. Mheshimu sana mtu anaekupa muda wake maana amekugawia sehemu ya maisha yake. Usimfanye aone amepoteza. Watu wengi huumia sana wanapopoteza pesa au vitu lakini hawashangai wala kuumia wala kujali pale wanapopoteza muda kwenye mambo yasiyo na maana.
Maisha yako ni Muda wako. Unapotumia muda vibaya unachezea maisha yako.
Success Kingdom
Jacob Mushi
+255654726668