Desmond Thomas Doss (February 7, 1919 – March 23, 2006) Alizaliwa nchini Marekani Virginia Alikuwa ni mwanajeshi aliepigana vita ya pili ya dunia. Katika Maisha yake alijiwekea ahadi kwamba kamwe hatashika bunduki hii ni kutokana na Imani yake kwamba kushika bunduki ni sawa na kuua.

Alipata upinzani mkubwa sana kwenye kambi ya jeshi wakati anafanya mazoezi na ilikuwa imebakia kidogo sana angefukuzwa. Alisema yeye yupo jeshini kwa ajili ya kuwasaidia wanajeshi wenzake wanaoumia vitani.

Watu wengi wakiwemo wenzake walimwambia kwamba atakufa vitani kwasababu hajui jinsi ya kutumia bunduki yeye anabeba biblia tu. Walipokwenda vitani wanajeshi wengi waliuawa wakiwemo viongozi wake lakini yeye hakulengwa na hata risasi moja.

Aliendelea na kazi yake ya kuokoa majeruhi wanaoumia kwenye vita. Aliweza kuokoa Zaidi ya majeruhi 75 kwa siku moja vitani ambao walisahaulika kwenye mapambano baada ya wenzake kukimbia.

Desmond Doss pamoja na kupingwa na kila mmoja aliweza kusimamia kile alichokuwa anakiamini na akafanya kile kilichomfanya yeye atamani kujiunga na jeshi.

Desmond Doss alitunukiwa tuzo ya Heshima kwa ujasiri wake wa kuweza kuokoa wanajeshi wenzake katika vita ile.

Viongozi waliokuwa wanampinga walikuja kumwambia hawakujua yeye ni mtu wa namna gani.

Tunaweza kujifunza hapa kwamba haijalishi watu watakupinga kwa namna gani kwenye ndoto yako endelea kuisimamia. Kile unachokiamini wewe ndio kitakuweka salama hapa duniani.

Kama huna unachokiamini utachukuliwa na upepo wa kila kinachotokea au unachoambiwa.

Soma: Upendo ni Kupoteza

Jiulize leo wewe ni kitu gani upo tayari kukisimamia? Kitu gani upo tayari kukipigania haijalishi utapingwa na wangapi, wakina nani? Kitu gani umeamua hutaondoka hapa duniani hadi kitokee?

Kama huna kitu unachokiamini na kukisimamia utaishi Maisha ya kuyumbishwa sana. Maneno ya watu yatakuwa yanakuumiza na wakati mwingine kukubadilisha.

Hakikisha kuna kitu upo tayari kukisimamia haijalishi ulimwengu mzima utakuwa kinyume na wewe. Watu wengi waliofanya mambo makubwa hapa duniani waliweza kwasababu ya vitu walivyoamua kuvisimamia na kuviamini.

Kuna wakati utafanya mambo utaambiwa hicho hakiruhusiwi lakini wewe unaamini kwamba ukikifanya kitaleta mapinduzi Fulani. Kama utashindwa kutetea na kusimamia hayo mapinduzi hayataweza kutokea.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading