Adui yako mkubwa wa mafanikio yako ya leo ni mafanikio yako ya jana. Vilevile mafanikio yako ya leo yanaweza kua sababu ya wewe kufanya kwa kiwango cha chini kesho.

Kua hai leo ni ili uweze kua bora zaidi ya ulivyokua jana kama kuna mambo ambayo ulifanya jana leo upande viwango zaidi.

Usiozee hali ya u kawaida binadamu hua tuna tabia ya mazoea Unafanya vitu kwa bidii ukishaanza kuona matokeo mazuri unaridhika kisha unajisahau.

Ni wakati wa kua bora leo hakikisha leo yako ni bora kuliko jana. Hakikisha utakachokifanya leo kizidi cha jana.

Haushindani na watu shindana na wewe mwenyewe.  Shindana na mafanikio yako ya jana.

Hakikisha jana haiipiti leo. Leo iwe bora kuliko jana.

Napenda kukutia moyo kua haijalishi unapitia changamoto za aina gani bado unahitaji kupanda viwango.

Panda viwango kwenye biashara yako, mahusiano yako, ndoa yako,  kiroho chako na Mungu wako.

Furaha yangu mimi ni kuona wewe unapiga hatua zaidi kwenda mbele kila siku. Hatua za ubora hatua za Mafanikio zaidi.

Kabla haijafika jioni jiulize;
Ni kitu gani Nitafanya au nimefanya cha tofauti na jana?  Chenye ubora wa juu zaidi kuliko jana?

Bila kua bora utajikuta unabaki pale pale.

Kumbuka: Kadiri unavyopanda viwango kila siku ndio unavyosogelea ndoto zako. Siku zote utakua unaamka na kulala masaa 24 kila siku.  Weka ubora kidogo kidogo hadi ufikie ndoto zako.
Hujamaliza mwendo ni hadi ufikie mauti. Usiridhike na hatua uliyofikia sasa.
Ni wakati wa kwenda hatua nyingine mbele.

Mwisho wako ni ile siku tunakuaga duniani.
Kumbuka Bwana yule aliejikusanyia mali na akiba ya chakula ya kutosha akaiambia nafsi yake;
“Ni wakati wa kupumzika ule na kushiba una chakula cha kutosha ghalani”
Usiku ule ule Akaambiwa “Mpumbavu wewe usiku huu tunaitaka roho yako.”

Usiridhike na kile ulichonacho. Usiridhike na hatua uliyofikia.
Kama bado upo hai ni wakati wa kwenda mbele zaidi.

Wako wazuri kuliko wewe na walishaondoka. Ni muda wa kufanya vitu vya tofauti katika maisha ya wengine.

Karibu sana
Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading