Chochote Unachokitaka kipo ndani yako.
Ili uweze kukipata unaanza kwa kuamini.
Unapoamini unakua na uhakika.
Imani yako itakua kutokana na matendo yako kila siku juu ya kile ukitakacho.
Imani ikiwa kubwa zaidi ndio unavyokaribia kufikia yale unayoyataka.
Heshimu na thamini sana kile ulichonacho sasa hivi maana ndio kinakusitiri leo. Asikudanganye mtu eti uchukie hali uliyonayo sasa. Mimi nakwambia yathamini maisha uliyonayo sasa furahia kipato unachopata sasa maana bila hicho usingeweza kuishi leo.
Kitu cha muhimu USIRIDHIKE NA HALI ULIYONAYO SASA.
Jacob Mushi
0654726668