Mara nyingi tumekua na tabia ya kukimbilia kufanya yale mambo ambayo tunaona ni rahisi kufanyika na pia yanawezekana. Tunajikuta tukikwepa yale mambo magumu yale ambayo yanaonekana hayaendi na kwa ufahamu wa kawaida hayawezekani.
Siri kubwa iliyopo ndani ya mambo haya tuyaonayo magumu ni kwamba mambo haya ndio yatakuwezesha wewe utoke hapo ulipo. Ukiweza kufanya yalisemwa hayawezekani lazima utoboe. Lazima ufikie kule ulikozani hakuwezekani.
Akili ya mwanadamu hua inapenda kujichagulia vile vitu ilivyovizoea. Unapoleta vitu vigumu inakwepa au itakuletea kuchoka na kujiona huwezi. Anza leo kufanya vitu vipya anza kuipa akili changamoto ya kufikiri mbali zaidi.
Fanya vitu ambavyo hujazoea kuvifanya nenda hatua nyingine zaidi ya pale ulipozoea kila siku. Siri kubwa utaiona ndani ya vitu hivi lazima uanze kupata matokeo ya tofauti. Lazima uanze kuona mabadiliko.
If you limit your choices only to what seems possible or reasonable, you disconnect yourself from
what you truly want, and all that is left is a compromise.
ROBERT FRITZ
Nakutakia weekend yenye furaha.
Jacob Mushi
0654726668
Sweet advice in the sweet moment
Karibu sana