#SiriZaKuaHaiLeo:1. Ni nafasi ya kubadilisha.

By | June 4, 2016
Ni nafasi nyingine ya kutubia makosa yako.

Ni nafasi nyingine ya kufanya upya kwa umakini pale ulipokosea jana.

Ni nafasi nyingine ya kufanya uchaguzi upya. Yako mambo mengi tumechagua jana kwa makosa mengine yana uwezekano wa kuchagua upya leo ndio wakati wake.

Ni nafasi nyingine ya kipatana na uliowakosea. Inawezekana jana umekwazana na watu leo hujawa hai kwa bahati mbaya. Ni wakati wako wa kutengeneza mambo na ndugu zako na marafiki uliokosana nao.

Ni nafasi nyingine ya kupanga kile unachokitaka kwenye maisha yako. Inawezekana bado hadi leo hujaweka malengo wala huna maono leo ni nafasi ya pekee kufanya hivyo usisubiri kesho.

Asante sana
Mushi Jacob

Leave a Reply