Unatakiwa kuwa na subira ili wakati wa kufanikiwa kwako huku ukijiandaa kupokea yale mafanikio yako.
Umejiandaa kwa kiasi gani?
Uko tayari kubeba kiwango gani?
Makwazo na changamoto utayaweza?
Kuna mengi utakutana nayo una kifua cha kubeba?
Lazima ujiandae katika lile unalolitaka kwasababu ukishindwa kujiandaa utajikuta unashindwa kubeba. Lazima uandae ufahamu wako kwa ajili ya mabadiliko yatakayotokea kwenye Maisha yako.
Ipo siku kweli usioijua mambo yatabadilika sana kuliko hata ulivyotarajia ila muda wa hayo mabadiliko kubakia kwako yatategemea na maandalizi uliyoweka.
Umejiandaa kupokea baraka?
Utaweza kubeba baraka zako?
Kuna nyakati baraka zako za miaka mingi iliyopita zinashindwa kuja Maishani mwako kwasababu tu huna maandalizi ya kutosha kuzipokea baraka hizo.
Kuna vitu vinazuiwa visitokee Maishani mwako kwasababu tu ukivipata hutaweza kuvibeba hivyo unasubiriwa ukue ili uweze kubeba zile baraka zako.
Hata mtoto ambaye hajakomaa hawezi kupewa mali zake za urithi kwasababu ni zake bali anapewa pale anapoonekana amekomaa na anaweza kumiliki mali zile.
Changamoto na majaribu unayopitia sasa hivi ni kipimo tu cha kuona je ni kweli unaweza?
Umekomaa?
Kadiri unavyolalamika unapopitia changamoto ndio unaonyesha kwamba bado hujakomaa kubeba zile baraka zako kubwa Zaidi.
Kuendelea kulia lia unapopitia changamoto ni mojawapo ya sababu ya wewe kukosa baraka kubwa Zaidi, utaendelea kupokea zile za kiwango ulichopo sasa hivi.
Kuza ufahamu wako, kuza uwezo wako ili upokee Zaidi yah apo ulipo sasa.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi,
Mwandishi, Mjasiriamali, Kocha wa Maisha, Mshauri na Mtaalamu wa Blogger ,
Instagram: jacobmushi
Facebook: Jacob Mushi Page
Barua pepe: jacob@usiishienjiani.com