Matendo yetu yote yanaongozwa na akili kama  akili zetu zitakuwa hazina afya basi tutakuwa tunapata matokeo mabovu kila wakati.

Unaweza kuendelea kulalamika kuwa hupati matokeo unayoyataka lakini nakusihi uanze kutazama akili yako huwa unaijaza vitu vya aina gani.

Kile kilichojaa sana kwenye akili yako ndio kinakuwa sababu ya matokeo unayopata. Mwaka huu punguza kabisa vitu ambavo havileti afya ya akili yako.

Acha kufuatilia umbea, sikiliza vitu ambavyo vinakuongezea Maarifa.

Punguza kuangalia Tv, usome vitabu Zaidi.

Acha kufuatilia mpira kupita kiasi na utumie muda huo kufuatilia biashara yako.

Kaa karibu Zaidi na Watoto wako kuliko unavyokaa karibu na simu yako.

Acha kufuatilia habari mbaya.

Acha kukaa baa ukilewa badala yake kaa karibu Zaidi na familia yako.

Acha kabisa kufuatilia Maisha ya watu kwenye mitandao ya kijamii halafu tumia muda huo kujifuatilia wewe Zaidi ujue unaelekea wapi.

Ukishindwa kuitumia akili yako vizuri basi akili yako itakuongoza wewe kwenda kufanya yasiyofaa. Anza sasa kujiongoza na kujilazimisha kufuatilia yale ambayo yanakufanya uwe bora Zaidi na Zaidi.

Chochote ambacho unakifanya kwa ugumu maana yake ni kwamba kwenye akili yako hakipo ndio maana unateseka. Hivyo basi cha kufanya ni wewe kuhakikisha akili yako inakikubali kile kitu  na hii itakuja kwa wewe kurudia rudia hadi akili izoee na kuona ni kitu cha kawaida.

Hakikisha kila siku unapiga hatua na kusonga mbele.

Jiunge na Mtandao wetu uwe unapokea makala hizi moja kwa moja kwenye email yako. Mwishoni mwa makala hii kuna sehemu ya kuweka email na chini yake pameandikwa Subsrcibe. Weka email kisha Bonyeza Subscribe.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Kocha Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading