Unaweza kumdanganya kila mtu kadiri ya uwezo wako lakini yupo mtu mmoja ambaye siku zote atakuwa anakutazama na kusikitika kwa kile unachokifanya na mtu huyu ni wewe. Unaweza kujaribu kukwepa watu ambao umewafanyia ubaya, ukawakimbia wanaokudai, ukawakimbia wanaokusema vibaya lakini wewe binafsi huwezi kujikwepa.

Hivyo basi mtu ambaye unapaswa kuhakikisha anakuwa mtu mwema, anaewapenda wengine, anaewajali wengine. Asiye na tabia mbovu ni wewe mwenyewe kbala hata hujawarushia wengine jiwe. Wewe ndio mtu wa kwanza unapaswa kuhakikisha umekuwa safi kabla hujataka Watoto wako waache tabia mbaya.

Wewe ndie mtu wa kwanza ambaye unaweza kuona makossa yako na ukawa na uhakika nayo kabla ya wengine. Hivyo basi mtu ambaye unapaswa kutumia muda mwingi kumfuatilia na kuhakikisha anakuwa bora ni wewe mwenyewe.

Ukirudi nyumbani acha kujikwepa acha kunywa pombe ili ujikwepe, acha kufuatilia habari ili ujikwepe. Unajua ale ambayo unajaribu kuyakwepa ndani yako yatakuja kukuletea madhara baadae na yatadhihirisha wewe ulivyo. Haijalishi ulikuwa unaigiza Maisha zile tabia ambazo umekuwa unazikimbia ndani yako na kujaribu kuzificha ipo siku zitakuabisha.

Unaweza kutumia kila njia ya kujikwepa kama kulewa, kuangalia habari, kuvuta sigara, kufuatilia Maisha ya wengine lakini bado utaendelea kuteseka. Sasa kwanini uteseke? Kwanini basi usitumie muda huo kuhakikisha unakuwa mtu bora?

Nakuachia kazi hiyo Rafiki yangu, achana na pombe, achana na sigara, achana na wanawake/wanaume. Tumia muda mwingi kujitengeneza wewe uwe mtu bora. Kabla hujaanza kuwagombeza wanao kwa tabia mbaya walizonazo anza wewe kujigombeza na uhakikishe una tabia ambazo wanaweza kuziiga.

Jiunge na Mtandao wetu uwe unapokea makala hizi moja kwa moja kwenye email yako. Mwishoni mwa makala hii kuna sehemu ya kuweka email na chini yake pameandikwa Subsrcibe. Weka email kisha Bonyeza Subscribe.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading