Unapokuwa mtu wa mawazo hasi unaweza kupita mahali ukawakuta watu wanacheka halafu ukaanza kuhisi kwamba wanakucheka wewe. Pia unaweza kuwakuta mahali watu wanazungumza kisha walipokuona wakanyamaza wewe kwasababu huwa unafikiri hasi tu kila saa unaanza kuhisi hawa watu walikuwa wananisema mbona wamenyamaza waliponiona?

Mtu mwenye fikra hasi anaishi Maisha ya tabu sana, anateseka kila wakati. Anaishi kwa hofu na mashaka kwa kuhisi watu wanamfikiria vibaya kwenye kila anachokifanya. Ni vizuri Rafiki ufikie kiwango ambacho hujali kabisa watu wengine wanachofikiria juu yako kwasababu hilo huwezi kulidhibiti.

Ukiwa mtu mwenye fikra chanya utakuwa na afya njema, akili yako itakupelekea kuona mazuri tu kwa wengine.

Akili yako na moyo wako utakuwa mweupe mara zote.

Huwezi kuwa na hisia mbaya juu ya wengine mara kwa mara.

Utajenga mahusiano mazuri na wengine kwasababu wakati wote wewe utakuwa ni mtu wa kutabasamu.

Huwezi kugombana na wat umara kwa mara kwasababu unachagua kufikiri chanya tu. Hata ukikosewa hutamuona yule aliekukosea kama mtu mbaya hivyo bado utataka kuona amani.

Chagua kuwa mtu anaefikiri chanya kwasababu ndio mwanzo wa kuvutia mazingira chanya kwa mafanikio pamoja na watu ambao watakuwa msaada kwako. Sio rahisi kuishi bila watu wenye maudhi lakini ukiweza kuwa chanya utaweza kuishi mahali popote pale.

Kuna msemo unasema mtu akikutukana kinachofanya lile tusi liwe bay asana na kukuletea hasira ni fikra zako wewe. Ile hali ya wewe kuanza kujifananisha na lile tusi ndio inakuongezea hasira halafu unajikuta umetaka kupambana na aliekutusi au kumtukana pia. Mtu akikutukana na wewe ndani yako una fikra chanya utatabasamu kwasababu unajijua wewe ni nani na wewe sio nani. Utamshangaa kwasababu hakujui vizuri ndio maana amekuita lile tusi.

Fikra chanya ni kwa afya yako, afya ya akili, mwili na roho yako pia. Fikiri chanya wakati wote.

Jiunge na Mtandao wetu uwe unapokea makala hizi moja kwa moja kwenye email yako. Mwishoni mwa makala hii kuna sehemu ya kuweka email na chini yake pameandikwa Subsrcibe. Weka email kisha Bonyeza Subscribe.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

ww www.jacobmushi.com/coach

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading