Ukisema huna mtaji wa kuanza biashara, hayo ni matatizo yako hakuna anaehusika sio mzazi wala serikali.

Ukisema mambo ni magumu kwako hayo pia ni matatizo yako Rafiki, njia pekee ni wewe kutafuta suluhisho na sio kuwabebeshea wengine.

Serikali haihusiki kwenye matatizo yako binafsi, unaweza kusema hapa kwamba kuna namna inahusika kwasababu mbalimbali ambazo unatoa lakini bado hizo sababu hazitasaidia.

Usitegemee kuna siku hali itakuwa nzuri na ukiwaza tu kupata hela basi zinakuja, kila wakati hela inatafutwa kwa nguvu kwa kuumia na kwa kutoa jasho. Ambao unawaona kama hawatoi jasho sana lakini wana pesa basi kuna kipindi waliteseka na kuumia hadi wakafika hapo walipo.

Kama mpaka sasa unasema huna mtaji, lakini hujafa njaa utakua unachekesha kwasababu kama huna hela ya biashara basi hata ya kule ungekosa.

Kama mpaka sasa bado unailalamikia serikali au ndugu zako ndugu yangu kwanza hakuna anaekusikiliza na wala hakuna anaejali na atakaekuja kujibu malalamishi yako.

Inuka hapo ulipo nenda katatue matatizo yako, nenda katafute pesa, ni kweli unaweza kusema ni jukumu la wazazi kuacha urithi kwa Watoto wao, sasa kama hawajakuachia wewe utafanyaje? Unaweza kusema serikali inapaswa kutengeneza mazingira Rafiki kwa vijana ili wajiajiri sasa kama haijatengeneza hao mazingira wewe utasubiri mpaka lini?

Muda haukusubiri, muda haujali kama wewe ulizaliwa maskini, uko kwenye nchi ambayo haina fursa, au yenye umasikini. Muda unakwenda na utashangaa kesho kutwa umeanza kuzeeka. Watoto wako nao wataanza kuishi Maisha yale yale uliyoishi wewe wakilalamika tena. Amka sasa nenda kabadilishe Maisha yako Rafiki yangu.

Jiunge na Mtandao wetu uwe unapokea makala hizi moja kwa moja kwenye email yako. Mwishoni mwa makala hii kuna sehemu ya kuweka email na chini yake pameandikwa Subsrcibe. Weka email kisha Bonyeza Subscribe.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

4 Responses

Leave a Reply to Gladys SimtituCancel reply

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading