Asilimia kubwa ya watu hupanga malengo mengi wanapoanza mwaka lakini inapofika katikati ya mwaka unawakuta watu wale wale wameshaacha kabisa vile vitu walivyopanga kufanya na kufanya vingine vipya ambavyo hawakupanga kabisa. Hii inasababishwa na kukosa hamasa, kukata tamaa kidogo kidogo na kujikuta umeanza kuvutiwa na jambo jingine ambalo umelisikia.

Unaweza kuanza malengo yako kwa hamasa kubwa sana, na baada ya muda Fulani nguvu ikaanza kupungua. Kadiri unavyokutana na ugumu Fulani kuna hamasa kidogo inapungua hivyo baada ya muda Fulani unaanza kuwa wa kawaida na unakosa nguvu tena za kuendelea.

Ipo njia moja ya kuweza kuziamsha tena nguvu zako na hamasa Zaidi ili usije kujikuta umeishia njiani. Unapaswa kuyasoma malengo yako kila siku na kuyaandika upya. Kama hutaweza kujipa kazi hii ya kusoma na kuandika upya malengo yako siku zote utajikuta unaanza vitu na huvimalizi. Unapanga malengo makubwa na unashindwa kufika nayo mwisho.

Unajua unapowaza kitu kwa mara ya kwanza kunakuwa kuna mambo mazuri sana unayaona. Unapoanza kufanya ukakutana na ugumu kidogo unaanza kusahau yale mazuri uliyoyaona mwanzo na kufikiria ugumu pekee. Sasa kama utakuwa una tabia a kusoma malengo yako kila siku lazima utaifufua upya ile nguvu. Lazima utaanza kuona upya yale mambo mazuri ambayo yalikupa hamasa mwanzoni ili kuchukua hatua.

Rafiki ili uweze vitu hivi unapaswa kuwa na watu ambao wanafikiri kama wewe na wana ndoto kubwa. Hawa pia watakuwa ni chanzo kingine ambacho kitakuongezea hamasa ya kuendelea mbele Zaidi. Karibu uwe pamoja na familia ambayo itakupa hamasa Zaidi.

Jiunge na Mtandao wetu uwe unapokea makala hizi moja kwa moja kwenye email yako. Mwishoni mwa makala hii kuna sehemu ya kuweka email na chini yake pameandikwa Subsrcibe. Weka email kisha Bonyeza Subscribe.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading