Usimcheke mtu kwa hali yeyote anayopitia kwenye maisha yake. Hata kama imechukua muda mrefu usinene mabaya yeyote juu yake.

Kuna nyakati unapitia bila kujua, kumbe ni Mungu anakuandaa ili uweze kuwa vizuri sehemu anayotaka akupeleke (kwenye kusudi lake).

Musa hakwenda kuishi kwa Faraoh ili ale bata, au asiuwawe. Alipitia kule ili ajifunze uongozi ili aje kuwaongoza wana wa Israeli Jangwani. Miaka yote aliyokuwa anaishi kwenye Kasri la kifalme alikuwa anajifunza sharia na vitu mbalimbali vinavyohusu utawala. Isingekuwa rahisi akaja akaomba kuingia kwa mfalme akiwa bado ni mtumwa. Kusudi la yeye kwenda kuishi kwa Faraoh halikuwa kuepuka kifo bali kujifunza uongozi na utawala. Utakuwa unakosea kama hutajua kwanini upo hapo ulipo sasa hivi.

Haikutokea pia kwa bahati mbaya Musa kumuua Mmisri ilikuwa lazima ili aweze kuondoka na kwenda kwenye hatua nyingine ambayo Mungu alitaka kumuandaa nayo. Wakati mwingine unaweza kujikuta umefanya kosa ukafukuzwa usilaumu, usijione wewe ni mzembe jaribu kujiuliza hili kosa ni kwasababu gani limetokea huenda ulitakiwa uondoke hapo ulipo kwasababu muda wako umekwisha.

Musa asingepigana na kumuua ule Mmisri asingepata sababu ya kukimbia na kwenda kule Midiani na kujifunza Maisha mengine ambayo Mungu alitaka ajifunze kule. Hivyo basi changamoto nyingine hutokea kwenye Maisha yako ili kukuinua viwango vingine Zaidi. Changamoto nyingine huja ili kukuhamisha sehemu moja uliokuwa umeshaizoea na kukupeleka sehemu nyingine mpya kwa ajili ya KUSUDI LA MUNGU.

Hivyo basi lolote linaloendelea kwenye maisha yako sasa hivi. Usikubali kujilaumu, Mungu anakuandaa. Watu wanaweza wasikuelewe, watasema unateseka lakini Mungu anakufundisha na kukutengeneza kwa ajili ya kazi yake.

Usiogope Tafuta kujua Sababu ya Mahali Ulipo sasa hivi. Muulize Mungu unataka nijifunze nini?

Jiunge na Mtandao wetu uwe unapokea makala hizi moja kwa moja kwenye email yako. Mwishoni mwa makala hii kuna sehemu ya kuweka email na chini yake pameandikwa Subsrcibe. Weka email kisha Bonyeza Subscribe.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading