SURA YA 436; Usiwe Kigeugeu.

jacobmushi
2 Min Read

Ukishajua unachotaka hupaswi tena kuwa na hofu yeyote kwamba itakuaje. Leo unasema unataka hiki kesho ukiona wenzako wamefanya kitu kingine wakapata matokeo ya haraka unataka kuacha ili na wewe ukafanye kama wao.

Wewe endelea mbele kwenye kile ambacho ulichoamua kukifanyia kazi na ukiweka juhudi za hali ya juu. Usiogope ugumu maana hakuna sehemu ambayo ni rahisi, wote unaowana wamefikia hatua Fulani ya kuvutia hawatakuonesha adha walizopitia, huenda zikawa ngumu kuliko hiyo unayotaka kuikwepa.

Usikubali kukimbizana na kila kitu kwasababu unaona matokeo ya haraka. Ukiwaangalia wale uliosoma nao na ukasikia walipofika kimaisha unaweza kujiona wewe hakuna cha maana ulichofanya. Ukweli ni kwamba wanadamu wanapenda kutumia kipimo kimoja kuwapimia watu wasiofanana. Wanapima uwezo wa mtu kwa kutumia kipimo kimoja.

Kama umeamua kwenda nenda usianze tena kujaribu kutazama kule ulipotoka wala kukumbuka yale mazuri ya zamani. Unajua wana wa Israel walipofika Jangwani walipatwa na njaa na kiu wakaanza kukumbuka vyakula walivokula kwa uhuru Misri. Ukweli walikuwa wanakula vizuri lakini walichosahau ni kwamba walikuwa watumwa.

Changamoto unazopitia zisikufanye ukumbuke kule ulipokuwa kifungoni. Pamoja na kwamba sasa hivi kuna ukame Fulani unapitia, labda umeishiwa fedha au umetengwa , wewe itazame Kaanani unayoelekea usikumbukie Misri. Misri ni utumwani na Kaanani ni kwenye uhuru wako. Usiwe kigeugeu na kukumbuka vile ambavyo ulishaamua kuviacha.

Jiunge na Mtandao wetu uwe unapokea makala hizi moja kwa moja kwenye email yako. Mwishoni mwa makala hii kuna sehemu ya kuweka email na chini yake pameandikwa Subsrcibe. Weka email kisha Bonyeza Subscribe.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading