Kama watu wangekuwa wananunua vitu kwasababu ya ukubwa au wingi wake basi mawe yangekuwa na thamani kubwa kuliko dhahabu. Hii inamaanisha kuwa haijalishi wewe una uzuri wa namna gani kwa sura yako kama huijui thamani yako utakuwa huna maana. Mtu anaevutwa kwako kwasababu ya muonekano wako wa nje akikaa na wewe baada ya dakika tano je atatamani kuendelea kukusikiliza?

Najua utakuwa ulishawahi kununua tunda ambalo linaonekana ni zuri sana kwa nje, linaweza kukusababisha utokwe na udenda. Halafu umetoa pesa yako kununua unafika nyumbani unakuta limeoza au halina ladha kabisa, huwa unajisikiaje? Unajisikia kama ulipoteza pesa yako.

Kitu ambacho wewe kama mwanadamu unapaswa kukifahamu baada ya kujua kusudi lako ni thamani yako. Wewe thamani yako ni ipi? Kitu gani ambacho unakitoa na watu wanakulipa nacho? Thamani yako sio vyeti vya chou hapana ni kile unachokijua. Kile ambacho watu wanakihitaji ili wakulipe.

Ukishaijua thamani yako bado haitoshi unapaswa tena kuanza kuhakikisha thamani yako haishuki au haipungua kadiri inavyotumika. Unaju ukinunua simu dukani laki tano halafu ukaitumia baada ya mwezi mmoja huwezi tena kuiza laki tano, thamani yake inashuka. Sasa wewe ni mara ngapi umetafuta namna ya kuongeza thamani yako?

Kuongeza thamani yako na kuilinda ni kuhakikisha unajifunza vitu vipya kila wakati. Sio lazima uende shule tena hapana unaweza tu kujiendeleza kwa kujifunza vitu mbalimbali ambavyo umeona vinafaa katika kuongeza thamani yako.

Njia ya kuilinda thamani yako ni kuhakikisha unajifunza kila wakati na sio kuzuia kutoa thamani yako. Toa lakini hakikisha unapotoa umeingiza vitu vipya maradufu ndani yako. Hii itakusaidia wewe uendelee kuonekana bora kila wakati kwenye kile unachokifanya.

Kinachowafanya wengi wanapotea baada ya kupata mafanikio makubwa ni kusahau kuongeza thamani yao. Unapobakia na vitu vile vile vilivyosababisha ufanikiwe jana sio rahisi leo ukafanikiwa Zaidi ya jana. Hakikisha kila siku unaongeza kitu kipya.

Jiunge na Mtandao wetu uwe unapokea makala hizi moja kwa moja kwenye email yako. Mwishoni mwa makala hii kuna sehemu ya kuweka email na chini yake pameandikwa Subsrcibe. Weka email kisha Bonyeza Subscribe.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading