Kuna watu ukiwatazama kwenye mitandao ya kijamii unaweza kutengeneza picha Fulani ya Maisha ambayo wanaishi na ukaanza kujiona wewe si kitu kabisa. Ukaanza kuona wewe umeachwa sana nyuma na wenzako Maisha yao yako viwango vya juu sana.

Ukweli Rafiki ni huu inawezekana ni kweli kabisa wanachoweka mitandaoni ni Maisha yao, sasa wewe ukiumia kuna kitu kinabadilika? Mfano sasa umeanza kujikuta unapata msongo wa mawazo ukaanza kutamani na wewe ufikie viwango vyao halafu baadae unajikuta kumbe uliacha Maisha ambayo ni bora sana kwasababu ya picha tu.

Ninachotaka kukwambia hapa ni wewe uachane na picha za Maisha ya watu. Anza sasa kuyafanyia kazi yale Maisha yako unayotaka wewe. Picha unazoziona mitandaoni zisikufanye uumie bali zikupe hamasa ya kufanya Zaidi na kupata matokeo makubwa Zaidi ya unayoyapata sasa.

Sio kama unavyofikiri kwasababu uhalisia ni wao wenyewe wanao. Wewe unaweza kutengeneza picha kubwa sana ambayo sio kweli halafu ukawa unateseka bure. Muhimu jitambue wewe ni nani halafu unaweza kutoa thamani ya aina gani kupitia wewe na watu wakulipe. Andika malengo yako makubwa ya kifedha ambayo unataka kuwa nayo halafu anza kufanya kazi kwa bidii hadi uyatimize.

Usikubali kupoteza furaha yako kwasababu ya kile ambacho unahisi umekosa kwenye Maisha yako. Unatakiwa ujue kama huna sasa basi ni nafasi yako wewe kuendelea kutafuta hadi upate. Kuwa chanya na chochote kile kichukulie kwa mtazamo chanya.

Ifundishe akili yako kufikiri chanya kwenye kila jambo unalopitia kwenye Maisha yako.

Jiunge na Mtandao wetu uwe unapokea makala hizi moja kwa moja kwenye email yako. Mwishoni mwa makala hii kuna sehemu ya kuweka email na chini yake pameandikwa Subsrcibe. Weka email kisha Bonyeza Subscribe.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

2 Responses

Leave a Reply to Jacob MushiCancel reply

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading