SURA YA 439; Tabia 6 za Kuacha Mara Moja Ili Usonge Mbele.

jacobmushi
By jacobmushi
3 Min Read
  1. Kupuuza Vitu.

Moja ya tabia ambayo nimekuwa naiona kwa watu wengi na ni mbaya san ani kupuuzia vitu. Yaani unaoneshwa kitu na bado hutaki kuchukua hatua yoyote hata ya kuuliza tu ili upate ufahamu. Kupuuzia kunaletwa na kujiona wewe unajua au kumdharau yule ambaye anataka kukuonesha au kukulekeza kitu. Ukiwa mtu wa hivi ipo siku utapuuza hadi watu wa muhimu kwako bila kujua.

2. Uvivu.

Unafanya jambo pale unapojisikia kufanya , ndugu yangu unategemea kufika kwenye unakokwenda? Embu fikiri upo kwenye mbio na wenzako halafu unaamua kutembea unategemea utashinda kwa muujiza? Kama hutaacha uvivu Rafiki utaendelea kuwatazama walioko mbele yako.

3. Kujiona Umeshajua Kila Kitu.

Nakumbuka nilipokuwa darasani kuna mwanafunzi mmoja alikuwa hamsikilizi mwalimu vizuri kwasababu alifikiri yeye anajua kila kitu. Sasa siku moja mwalimu katoa maelekezo ya namna ya kujibu maswali yeye akawa hasikilizi mwishoni akaja kufeli mtihani kwasababu tu hakufuata maelekezo alijibu vile alivyokuwa anataka yeye.

Kwenye Maisha ukiona wewe umefika mahali unaona unajua kila kitu, hujajifunza kitu vizuri tayari umeshakimbilia kufanya utaishia kuanguka na kuishia pabaya. Unapofundishwa kubali kusikiliza maelekezo mpaka mwisho, kubali kuwa mwanafunzi. Usijifanye unajua mbele ya mwalimu wako bora ufanye hivyo mbele ya wanafunzi wenzako.

4. Kutumia Hisia Kwenye Mambo Yanayohitaji Kufikiri.

5. Tamaa Mbaya.

Unatamani vitu ambavyo hujavitolea jasho, mfano wewe ni mdada unataka kutumia uzuri wako ili upate upendeleo Fulani. Hiyo haitakusaidia itakufanya uje kuwa mtumwa tu. Unataka vitu vya haraka haraka ambavyo hujui vimetoka wapi. Mtego wa panya pekee ndio una chakula cha bure.

6. Ubinafsi

Hapa ni pale unamsumbua mtu unapohitaji jambo Fulani ukishalipata basi hakuoni tena. Halafu sasa yeye akiwa na shida unaanza kujifanya upo bize au hata hupokei simu, ndugu yangu hayo mambo hayafai kwa sasa. Ukiwa mtu kuangalia faida unazopata wewe tu halafu hutoi ushirikiano kwa wengine unajitengenezea shimo. Watu watakukimbia.

Jiunge na Mtandao wetu uwe unapokea makala hizi moja kwa moja kwenye email yako. Mwishoni mwa makala hii kuna sehemu ya kuweka email na chini yake pameandikwa Subsrcibe. Weka email kisha Bonyeza Subscribe.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading