Tabia ya kujifunza na Kusoma vitabu inahusika katika kukuletea mafanikio.

jacobmushi
By jacobmushi
5 Min Read
Habari za leo ndugu. Natumaini unaendelea vyema na kupambania kufikia ndoto yako na maisha bora. Tunaendelea na mfululizo wetu wa Makala za tabia. Kwanini tabia? Maisha ya mwanadamu yanajengwa na tabia ndogo ndogo tulizozitengeneza kila siku huko zamani. Na kwa kawaida kila siku kuna tabia mpya unaanza kuitengeneza polepole iwe kwa kuiga kwa wengine au kutokana na mazingira unayoishi. Hivyo basi unaweza kuondoa tabia yeyote ambayo huipendi na kujitengenezea tabia nzuri ambazo zinavutia mafanikio.

 
 
Kwanini kujisomea vitabu? Hii ni tabia moja ambayo watu hua wanalalamika sana kwamba Watanzania hawapendi kusoma vitabu ni kweli ndio maana bado ni masikini sana. Muasisi wa taifa hili alikua na tabia ya kusoma vitabu sana ndio maana aliweza kuongoza kwa hekima kuu na kuacha alama ambayo haitasahaulika. Tunaona viongozi wetu wengi wakifanya mambo ya ajabu wakiongea vitu visivyo eleweka hii yote ni kwasababu hawakujiandaa kwa kusoma na kujifunza. Haijalishi unataka kuja kua nani kusoma ni muhimu sana kwani kutakusaidia wewe uweze kua imara kule unapoelekea.
Kwa kupitia kusoma vitabu tunakua tunayaishi maisha ya watu miaka iliyopita. Ukitaka kukutana na watu maarufu sana waliokuwepo zamani unawapata kwenye vitabu. Ukitaka kujifunza kwa matajiri wakubwa duniani unawapata kwenye vitabu. Kusoma vitabu ni muhimu sana kwenye maisha yako.
 
“A reader lives a thousand lives before he dies, said Jojen. The man who never reads lives only one.” 
― 
George R.R. Martin,
Mwandishi huyu anasema  mtu anaesoma vitabu anaishi miaka elfu kabla hajafa, lakini asiejisomea anaishi mara moja tu. Kwanini? Kwa kupitia vitabu unayaona misha ya watu wengi sana na kujifunza kwao.
A man only learns in two ways, one by reading, and the other by association with smarter people. Will Rogers
Tunajifunza kwa njia mbili, kwa kusoma vitabu na kwa kutembea na watu nadhifu.


Learning is the beginning of health. Learning is the beginning of spirituality. Searching and learning is where the miracle process all begins.” – Jim Rohn 
Kujifunza ndio mwanzo wa afya, kujifunza ndio tunakua kiroho. Kutafuta na kujifunza ndipo miujiza yote huanzia.
 
“Formal education will make you a living; self-education will make you a fortune.” 
― 
Jim Rohn
Hakuna namna unaweza kufikia mafanikio makubwa kama hujifunzi kama husomi vitabu kila siku. Nionyeshe mtu mmoja unaemfahamu aliefanikiwa na hasomi vitabu ni mvivu wa kujifunza. Sidhani kama utampata mtu huyo na ukimpata atakua ni maskini.
Ulimwengu wa sasa umebadili na umerahisisha njia za kujifunza. Unaweza kujifunza vitu vingi sana kupitia mitandao hii kama unavyosoma Makala hizi. Unaweza kusoma vitabu kwa njia nyingi sana. Kupitia simu yako ya mkononi.
 
Kama unafikiri wewe ni mvivu wa kusoma kuna audio books vitabu vilivyosomwa unaweza kujifunza kwa kusikiliza. Simu yako ya mkononi unaweza kujifunza nayo mambo mengi sana. Jiunge na watu wanaopenda kusoma. Kama wewe unatamani kusoma vitabu na unakaa na watu ambao mar azote wanapenda kuangalia movie hutakaa uweze kujisomea. Tafuta makundi ambayo yatakuvutia kwenye kujisomea.
Hakikisha popote pale ulipo una kitabu, umesafiri safari yeyote uwe na kitabu mkononi au kwenye simu yako.  Nakuhakikishia kwamba unayojifunza sio bure unajiandalia baadae yenye furaha na Amani. Unajitengenezea maisha yenye mafanikio.
 
Acha kupoteza muda kufuatilia vitu visivyo na maana kwenye maisha yako. Lisha ubongo wako chakula chenye manufaa na ubongo utakuletea matokeo bora sana huko baadae. Unataka kua mtu maarufu sana, kiongozi mkubwa sana, huwezi kupata hivyo bila kujitengenezea tabia ya kusoma vitabu.
Ukitaka kujitengenezea tabia yeyote hakikisha unafanya kwa kurudia rudia kwa siku 21 bila kuruka.
 
 

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi

#UsiishieNjiani

“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio… https://jacobmushi.com/patavitabu

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog ….. https://jacobmushi.com/jipatieblog

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp… https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading