Tabia ya Kutoa inavyohusika katika mafanikio yako.

Habari za leo rafiki yangu. Naamini unaendelea vyema na maisha yako. Ni siku nyingine tena ambayo tunajifunza tabia mbalimbali zinahusika katika kukuvuta kwenye mafanikio makubwa. Leo tunakwenda kutazama tabia ya Kutoa na Kupokea katika maisha yetu.

Kutoa, ni kitendo cha kupeleka vitu ulivyonavyo kwa jamii inayokuzunguka. Iwe umetoa kitu kama msaada au umetoa kitu ili urudishiwe kingine yote ni kutoa. Unapokwenda unataka sukari kilo moja na una pesa ya nusu kilo huwezi kupata sukari. Unapokea kulingana na ulivyotoa. Kadiri unavyotoa kwa wingi ndivyo unapokea kwa wingi. Huwezi kutoa kitu ambacho huna. Ili uweze kupokea vikubwa na vyenye thamani Zaidi unatakiwa uongeze thamani yako. Thamani yako inapokua juu unachopokea nacho kinakua ni kikubwa. Unatoa nini kwenye jamii inayokuzunguka ili uweze kupokea?
Kabla hujaanza kulalamika kwamba huna pesa na hali ni ngumu hakikisha umefahamu kwamba ili upate pesa lazima uwe umetoa kwenye jamii. Unaweza kutoa ujuzi wako, bidhaa, huduma, na vingine vingi. Wawezeshe wengine na wewe unakua kwenye nafasi ya kuwezeshwa na wengine.
“Utapata kila unachokitaka kama utaweza tu kuwasaidia watu wengi Zaidi kupata kile wanachokitaka” Zigg Ziglar.
Ili uweze kufikia mafanikio makubwa lazima uwe unawaza kutoa Zaidi kuliko unavyopokea. Kadiri unavyotoa kwa wingi unajitengenezea nafasi ya kupokea vingi sana.

GIVING BACK TO THE SOCIETY.
Jijengee tabia ya kutoa kwenye jamii mfano unaweza kuwasaidia wasiojiweza kwenye kila kipato unachokipata. Unaweza kutenga 10% ya kipato chako kwa ajili ya kuwasaidia watu mbalimbali duniani. Ukifanya hivyo utajikuta unapokea Baraka za Mungu na fursa zitafunguka kila kona. Matajiri wote duniani hua wanatabia hii ya kuwasaidia wasiojiweza ndio maana tunaona misaada mbalimbali kutoka nje kwa nchi maskini huku Africa, wanasaidia yatima, wanasaidia wagonjwa wa ukimwi, na wengine wengi ndio maana mafanikio kwa hayaishi. Hivyo ni vyema na wewe ujijengee tabia hii ya kuwasaidia wengine  bila hata wengine kujua. Msaada wa kweli sio ule wa kupiga kelele kila mtu ajue umetoa sehemu Fulani kwa ajili ya maskini.

Toa bila kutarajia chochote.
Unapotoa kwa nia ya kumsaidia mtu mwenye shida usitarajie chochote kutoka kwake au popote pale. Toa halafu sahau. Ukifanya hivyo utajikuta unapokea hata bila kujua vitu vinatoka wapi. Maneno wanayonena juu yako wale uliowasaidia yanavuta mafanikio kwako unajikuta kila unachokifanya kinaleta matokeo makubwa.
Haijalishi unakipato gani kutoa iwe tabia yako hata ukipata Tsh 10,000 hakikisha unaweka fungu la kutoa kwenye jamii. Na hii ni tofauti kabisa na pesa unayopeleka kule unaposali.
Ukijijengea tabia hii ya kutoa utaniambia mwenyewe matokeo yake. Baraka zitakufuata hadi utashangaa mwenyewe. Ila kumbuka toa bila kutarajia chochote, usitoe ili ubarikiwe toa kutoka moyoni kwa nia ya kusaidia wengine ambao hawana.
Karibu sana
Siri 7 za Kua Hai Leo
0654726668

Jacob Mushi.
jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading