Unaweza kujenga Tabia nyingine nyingi mbaya au nzuri kwa kufanya mara kwa mara. Kwa kurudiarudia kila siku. Angalia ni vitu gani unavyofanya mara kwa mara na vina manufaa gani kwenye maisha yako kwa ujumla maana ni Tabia zinajengeka hizo.
Kama zilivyo tabia za kimaskini vile vile zipo tabia za watu wenye mafanikio makubwa. Ukiweza kufanya wanachofanya waliofanikiwa na wewe utafanikiwa, Ukifanya wanayofanya maskini na wewe utakua maskini.
Hizi ni baadhi ya tabia za waliofanikiwa sana.
Kuamka mapema.
Inawezekana wewe unafikiri kwamba ipo siku ukiwa na pesa nyingi utaamka muda unaotaka na kufanya unachotaka ni kweli si vibaya. Ila ili uweze kua na mafanikio makubwa jijengee tabia ya kuamka mapema angalau saa kumi na moja alfajiri. Hapa unapata muda mzuri wa kukaa na kutafakari maisha yako yanavyokwenda. Vilevile unapata muda wa kuipanga siku yako. Ufanye nini ili uwe na siku ya uzalishaji zaidi. Jijengee tabia hii ya kuAmka mapema.
Kusoma vitabu.
Watu wenye mafanikio makubwa wanasoma vitabu sana. Tena kila siku na hii ni tabia vile vile Inawezekana wewe toka umalize masomo yako hujawahi kupitia kitabu chochote hata cha dini yako. Unajijengea tabia ya kimaskini. Kwenye vitabu unakuza ufahamu wako na unakua na maarifa zaidi ambayo yataongeza kasi yako ya uzalishaji. Anza Kusoma vitabu leo kama una mipango ya kua na mafanikio makubwa. Ukijijengea tabia hii itakuletea mabadiliko makubwa hutakua mtu wa kawaida.
Kusikiliza
Watu wenye mafanikio makubwa wanatabia ya Kusikiliza kuliko kuongea zaidi unaposikiliza unajipa nafasi ya kujifunza zaidi kuliko ukiongea. Na kumbuka ukiongea sana upo kwenye hatari ya kukosea zaidi. Jaribu kua msikilizaji mzuri utajifunza mengi kutoka kwa wengine.
Shukrani
Watu wenye mafanikio makubwa wana tabia ya Shukrani tabia ya kushukuru inajengwa kwa kufanya mara kwa mara. Shukuru kwa ulichonacho ili uweze kupata vingi zaidi Acha kulalamika jiangalie kila siku una kitu gani ambacho Utamwambia Mungu asante. Na sio Mungu peke yake wapo watu wengi pia wamefanyika sababu ya wewe kupata unachotaka kwenye maisha yako onyesha Shukrani hii itakufanya wewe uendelee kupata zaidi. Maskini wanalalamika kama na wewe una hiyo tabia iache mara moja. Maskini wanalaumu wanatafuta watu wa kuwalaumu juu ya shida zao na umaskini wao kama una hiyo tabia acha mara moja.
Kutoa.
Tabia ya kutoa ni tabia nyingine ambayo itakufanya wewe upate zaidi ili uweze kubarikiwa lazima uwe na tabia ya utoaji. Na hapa sizingumzii sadaka peke yake kuna vitu vingi unaweza kutoa mfano umejifunza vitu vingi vizuri unaweza kuvitoa wengine wafahamu. Unaweza kujijengea tabia ya kutoa msaada kwa watu wasiojiweza. Na hii haina maana mpaka uwe na vingi ndio utoe hapana kama una shilingi elfu moja tenga shilingi mia ya utoaji wako watu hawawezi sehemu mbali mbali unaweza kufanyika baraka maishani mwao. Na kadiri unavyotoa ndio utapokea zaidi.
Asante sana kwa kujifunza pamoja nami fanyia kazi hizo tabia zitakuletea mafanikio.
Jacob Mushi
Mawasiliano 0654726668 Email jacob@jacobmushi.com