Habari rafiki, Umeanzaje siku yako? Umefanya mazoezi? Umesoma kitabu?
Kitu gani kinakutambulisha hapa duniani? Kama mpaka sasa unashindwa kujibu swali hili unahitaji msaada wa karibu sana. Kama binadamu unatakiwa uwe na kitu ambacho ni utambulisho wako wewe binafsi kwenye dunia hii.
Utambulisho wako ni kile kitu ulichoamua kukifanya hapa duniani hadi unakufa. Unamkumbuka msaani wa nyimbo marehemu Bibi Kidude? Hadi amezeeka kabisa bado alikua anaimba hii ni kwasababu kile ndicho alichoamua kukifanya na akata kiache alama kwenye dunia hii.
Wewe umechagua kitu gani? Kitu gani kinaugusa moyo wako Zaidi ya vingine? Kitu gani unataka usikie watu wakikutaja nacho? Amua sasa muda bado upo haijalishi una umri gani sasa hivi bado waweza kufanya mambo makubwa.
Utofauti wako na wanadamu wengine hapa duniani ndio utambulisho wako. Unajua simba ni simba tu yaani hawana kitu cha tofauti sifa zao wote zinafanana. Lakini sisi binadamu kila mmoja ana kitu chake cha pekee ambacho kipo ndani yake. Usikubali kabisa ukaondoka na hicho kitu ukiwa hujakifanyia kazi kabisa.
Embu jiulize leo ni kitu gani hasa utakijutia sana ukiondoka hapa duniani ukiwa hujakifanya? Iumize akili yako vya kutosha hadi upate jibu. Ukishapata majibu yaandike kwenye notebook yako. Yanaweza kuja majibu mengi lakini utaangalia moja kati ya majibu yote ni kipi kinaleta furaha Zaidi kwenye moyo wako.
Ni furaha yangu nione watu wengi wakigundua sababu za wao kuwepo hapa duniani. Ni furaha yangu nione watu wakitimiza ndoto zao hivyo kama wewe unasoma Makala hizi tafadhali sana zifanyie kazi ili uwe moja wapo ya matunda ya hiki ninachokifanya.
Utambulisho wako ni wa muhimu sana hapa duniani. Utambulisho wako ndio wewe hasa. Usikubali kuishi bila kutambua kinachokutambulisha.
Kuwa Mwanachama Kamili wa Usiishie Njiani Bonyeza hapa.. https://jacobmushi.com/jiandikishe/
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. https://jacobmushi.com/patavitabu/
Jipatie Blog Bora hapa.. https://jacobmushi.com/jipatieblog/
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
“Piga Hatua”