HATUA YA 190: Mambo ya Muhimu Ya Kufanya Unapoamka Asubuhi.

Vile unavyoianza siku yako inaweza kuwa sababu ya kuwa na siku mbaya sana au siku nzuri sana. Kuna makossa unaweza kuwa unayafanya bila kujua wakati unapoamka na yakaigharimu siku yako nzima. Kwanza lazima uamke mapema sana ili kuweza kuwa na siku nzuri. Unapochelewa kuamka na kuanza kukimbia kimbia kwasababu muda umekupita unakosa umakini wa kufanya […]

SIMAMIA UNACHOKIAMINI

Desmond Thomas Doss (February 7, 1919 – March 23, 2006) Alizaliwa nchini Marekani Virginia Alikuwa ni mwanajeshi aliepigana vita ya pili ya dunia. Katika Maisha yake alijiwekea ahadi kwamba kamwe hatashika bunduki hii ni kutokana na Imani yake kwamba kushika bunduki ni sawa na kuua. Alipata upinzani mkubwa sana kwenye kambi ya jeshi wakati anafanya mazoezi na ilikuwa […]

HATUA YA 154: Penzi Changa..

Inawezekana umeshangazwa na kichwa ambacho kinaenda leo. Ni kweli leo nataka tuangalie juu ya vitu ambavyo mara ya kwanza huanza kwa hamasa kubwa lakini ukishaanza kuingia katikati ndio unaanza kuupata ukweli halisi. Mara zote kitu chochote kipya huwa kinahamasisha sana. Wapenzi wanapoanza mahusiano siku za mwanzo wanafurahiana sana. Kila mmoja anaweza kumpa mwenzake ahadi ambazo […]

HATUA YA 130: Nguvu ya Uthubutu na Kuchukua Hatua

Jambo lolote unalotamani kulifanya linaanza na uthubutu wa kuchukua hatua ya kwanza, kama hutajaribu kuanza kupiga hatua hautaweza kwenda mahali popote. Mtoto mdogo anaweza kusimama kwa kuanza kusimama kidogo kidogo huku akiogopa na mara nyingine huanguka. Nakumbuka nilikuwa na mdogo wangu mmoja wakati akiwa mdogo aliogopa sana kutambaa, ikabidi tuwe tunamwekea kioo mbele yake. Anapojiona […]

VITU MBALIMBALI VYA KUFANYA ILI UWE NA UHURU WA KIFEDHA

Habari rafiki, kwenye maisha ya sasa ili uweze kuishi maisha yale ambayo unayotaka kwa zaidi ya 50% lazima uwe na njia mbalimbali za kukuingizia kipato. Usikubali kutegemea njia moja ya kukuingizia kipato. Hata kama sasa unategemea njia moja anza mpango wa kutengeneza njia nyingine kwa ajili ya vipato. Biashara nyingi kubwa zinaweza kujiendesha zenyewe na […]

Mambo 9 ya Kufanya ili Uishi Maisha yenye Furaha Siku Zote.

Habari ya leo rafiki yangu na msomaji wa Makala hizi. Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vyema na safari ya mafanikio. Katika Makala yetu leo nitakwenda kukushirikisha vitu 9 vya kufanya ili uweze kua na maisha yenye furaha. Kwenye maisha zipo  chngamoto nyingi tunazozipitia na zinasababisha tuishi maisha ya wasiwasi,huzuni na woga wa kesho ukiweza kufanya […]

Mambo uliyokuwa huyajui Kuhusu Ajira

Habari za Leo Msomaji wetu. Tunakwenda kuzungumzia kwa kifupi juu ya ajira na waajiriwa na jinsi ya kujitoa kwenye kongwa hili. Ni kweli tunategemeana katika maisha yetu mwenye biashara anategemea wafanyakazi ili aweze kukuza zaidi biashara yake. Lakini bado hiyo haitakiwi kuwa sababu ya wewe kutofanya kitu kingine na kubakia unategemea mshahara peke yake.  Mabadiliko […]

Nguzo 10 za Mafanikio

Habari za Leo ni matumaini yangu u mzima na unaendelea vyema. Leo tuanajifunza nguzo 10 za mafanikio yako. Ukiweza kuzisimamia nguzo hizi lazima utaona mabadiliko na kusonga mbele kuelekea kwenye ndoto zako. Karibu tujifunze pamoja mpaka mwisho. Jua kusudi la kuzaliwa kwako. Nguzo ya kwanza na ya muhimu sana ni wewe kutambua kwanini ulizaliwa. Upo […]

WEWE NI MSHINDI

Mshindi ni mtu alieshinda, Hivyo wewe ni mshindi kwa kua umeshinda, kua hai leo ni ushindi, kuwa na Mungu mpaka sasa huo ni Ushindi, kuweza kujifunza semina na kufuatilia mafundisho kama haya wewe ni mshindi. Embu jiulize ni watu wangapi ulikua unawafahamu leo hawapo duniani? Wewe umeshinda Mungu kakuweka duniani ili uendelee kushinda. KWANINI WEWE […]

MAMBO MATATU YA KUZINGATIA KILA SIKU

Habari za leo ndugu msomaji wa mtandao huu ni matumaini yangu kua ni mzima na unaendelea na shughuli zako vyema. Leo tunajifunza mambo matatu ya muhimu na ya lazima kua nayo ili uwe na furaha katika maisha yako nimejaribu kyatafakari sana nikagundua kua chanzo cha kutokua na furaha ni mtu kufanya mambo mawili na kuacha  […]