Tag Archives: ndoto yako

#HEKIMA YA JIONI: USIKUBALI KUWA MFUNGWA KWENYE FIKRA ZA WENGINE,

Unaweza kuwa na kila kitu ambacho wengine kwa nje wanaona ni kizuri lakini kumbe yote hayo ni matokeo ya mawazo ya watu wengine juu yako.

Kama unachokifanya hakijatoka ndani yako utaishi Maisha yako yatakuwa ni kifungo cha mawazo ya wengine .

Kutokana na maoni ya watu wengine juu ya Maisha yanavyotakiwa kuwa umejikuta upo ndani ya maoni yao na mawazo yao bila kujua. Uliambiwa kwenu lazima mtoto wa kwanza awe daktari na wewe ukaenda kusomea udaktari sio kwasababu imetoka ndani yako bali kwasababu ni mawazo ya watu wengine.

 

Tuna watu wengi wanakuwa waovu na wabaya kwenye kazi wanazozifanya kwasababu tu sio kitu walichozaliwa kuja kufanya. Kuna kazi ambazo wengi walikimbilia kufanya kwasababu tu Maisha yalishakuwa magumu kwao na wakakosa pa kwenda.

Unaweza kuwa na mshahara mzuri na kila kitu kizuri lakini kamwe huwezi kuwa na furaha hadi ujue ni kwanini upo hapa duniani.

 

Ukiona mtu anafanya mambo ya ajabu kwenye kazi yake lazima kunakuwa na matatizo. Hii ni kwasababu wengi wanafanya vitu ambavyo walilazimishiwa. Wengi wanafanya kazi kwasababu walikuta watu wanafanya kazi duniani.

Wengi wanaishi Maisha wanayoishi sio kwasababu ni sahihi bali ni kwasababu wamekuta binadamu wengine wanaishi. Hata kama kulikuwa na makossa yaliyokuwa yanaendelea toka zamani wanakuwa wanayaendeleza.

Jiulize maswali magumu juu ya kile unachokifanya je ni kweli umezaliwa uje kufanya? Ni bora ufanye jambo ukiwa unajua baada ya muda Fulani utaachana nalo na kuendelea na mambo mengine kuliko kuwa mtu asielewa kwanini anafanya. Wengi wanafanya kwa kufuata mkumbo na sio kwasababu wanachokifanya ni sahihi.

 

Lazima ukubali kujua Maisha unayoishi umefuata kama ulivyokuta wanaishi au ni namna ambavyo Mungu ametaka uje kuishi hapa duniani.

 

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

HATUA YA 301: Ukiweza Kuvumilia hiki Lazima Utimize Ndoto yako.

“If you don’t quit, and don’t cheat, and don’t run home when trouble arrives, you

can only win.” – Shelley Long

Zinapofika nyakati za matatizo kama uispoacha, usipofanya udanganyifu na wala usipokimbia kurudi kule ulipopazoea ni lazima ushinde. – Shelley Long

Hakuna hata sehemu moja umeona mtu ameacha kupambana au kufanya kile anachokifanya kwasababu kinamletea matokeo mazuri. Kila mmoja wetu atapenda kuendelea kufanya Zaidi na Zaidi kwasababu kuna matokeo mazuri. Lakini ili uweze kuwa mshindi kweli kweli ni lazima uonyeshe uimara na utayari wako wa kuendelea nyakati za matatizo na ugumu.

Kila mmoja atafurahia sana anachokifanya wakati mambo yanakwenda vizuri. Kila mmoja atajisiikia vizuri sana pale ambapo jioni akihesabu fedha anaondoka na faida kubwa. Lakini zile nyakati za huzuni ndizo zinaonyesha ukweli kama wewe ni mshindi.

Lazima ujue kuwa huwezi kufurahi nyakati zote. Kuna vipindi utapitia vitakuhitaji uwe mgumu usiekubali kushindwa.

Ndoto yako yako itakwenda kutimia tu pale ambapo utaamua kutokurudi nyuma bila ya kujali ni hali gani inaendelea. Kuna nyakati utajihisi upo peke yako lazima pia ukubali kuendelea kupambana bila ya kukata tamaa.

Wapo watu watakaokuja na kukwambia achana na hicho unachokifanya kwasababu wameona hakina maslahi. Kwako wewe unapaswa kujua ni kitu gani uliona wakati unaanza? Ile picha picha usikubali ififie moyoni mwako. Endelea kuitazama kila wakati unapokuwa kwenye hali ya kukata tamaa.

Nyakati pekee watu wanakata tamaa na kurudi nyuma ni nyakati ngumu. Na hizi ndio nyakati za kuchambua washindi wa kweli.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/