Tag Archives: nidhamu

HATUA YA 304: Usipoacha Tabia Hii..

  Wakati unaendelea kulalamika na kutoa sababu nyingi za kujitetea kwa hali uliyonayo sasa hivi: Bado una muda mwingi wa kutumia simu yako kuperuzi kila kinachoendelea mitandaoni. Bado una muda wa kutazama tamthilia ndefu kwa masaa kadhaa. Bado una muda wa kukaa sehemu na ukapoteza muda ukiwasema watu na serikali jinsi ambavyo haijakufanyia vizuri. Bado… Read More »

#HEKIMA YA JIONI: Kama Unavyoitaka Pumzi Ndivyo Unavyotakiwa Kuyataka Mafanikio.

Kulikuwa na kijana mmoja alikuwa anataka mafanikio sana. Akamfuata Mentor wake na kumuomba amuelekeze ili na yeye aweze kufanikiwa. Mentor wake akamwambia kesho tukutane ufukweni mwa bahari asubuhi. Yule kijana akajisemea moyoni mwake, “mimi nataka mafanikio na pesa lakini ameniambia tukutane ufukweni kwani nimemuomba anifundishe kuogelea?” akasema tena, “kwa vile nataka pesa na mafanikio nitakwenda.”… Read More »

HATUA YA 262:  Mambo 5 yatakayokufanya Uendelee Kubakia Hapo Ulipo.

Mara nyingi unaweza kukutana na mtu anasema “Ningekuwa na Mtaji wa shilingi fulani ningefanya biashara Fulani” sasa ukimuuliza mawazo yako ni mazuri sana sasa unafikiri huo mtaji unaousema unatoka wapi? Kuna juhudi gani unafanya sasa hivi ili angalau uwe na huo mtaji? Mtu huyo ataanza kukupa maelezo ya kutosha kwanini haiwezekani na hali ilivyo mbaya.… Read More »

HATUA YA 251: Madhara ya Kuupuzia Vitu Vidogo Vidogo.

Tofali hujengwa kwa mkusanyiko wa punje moja moja za mchanga ambazo unaweza kuzibeba mkononi mwako lakini hujenga tofali ambalo huwezi kulibeba kwa mkono mmoja. Tofali nalo hujenga ghorofa kubwa sana ambalo binadamu na mali nyingi za thamani hukaa humo. Hadi unaliona jengo kubwa la ghorofa linalotokea lilianza kwa mkusanyiko wa punje ndogo sana ya mchanga.… Read More »