Tag Archives: nukuu za mahusiano

527; HEKIMA: Kinyozi Anapokosea Kukunyoa.

Kinyozi anapokosea kukunyoa bila kujali amekosea kiasi gani siku zote baada ya muda Fulani nywele huota tena na utaweza kunyoa vile unavyotaka. Unapopoteza fedha haijalishi ni nyingi kiasi gani kama ni wewe mwenyewe ulizitafuta basi utaweza kuzipata tena.

Unapoachwa na mpenzi ambaye ulimpenda sana bila kujali alikuwa mzuri kiasi gani, bado ipo siku utakuja kukutana na mtu mwingine mzuri kuliko yeye na utampenda kuliko yeye. Ni wewe tu kuamua kwamba yaliyopita yapite uendelee na safari.

Kipo kitu kimoja kikitokea kwenye Maisha yako huwezi kubadilisha tena, kitu hicho ni KIFO. Unapokufa inakuwa ndio mwisho wako wa kufanya vitu hapa duniani. Huwezi tena kurudi kuja kubadilisha chochote. Na bahati mbaya sana baada ya kufa hakuna ajuae kinachoendelea au mtu anakuwa wapi.

Sasa nikuombe wewe ambaye upo hai usikubali jambo lolote ambalo linaweza kubadilishwa likuumize kichwa au likufanye ukate tamaa. Nataka ukumbuke kwamba ipo siku utakufa na hutopata tena hiyo nafasi ya kuanza upya uliyonayo sasa.

Dunia haina shida wala haijutii wewe ukifariki, kila siku wanazaliwa watu wapya ambao watakuja kufanya kile ambacho wewe ulishindwa kufanya. Sasa usikubali kuondoka hivi hivi, usikubali alama uliyotakiwa kuiacha ije iachwe na mtu mwingine.

Ndugu yangu kinyozi akikosea kukunyoa kumbuka kwamba nywele zitaota ten ana utakuja kurekebisha vile unavyotaka. Lakini siku ukiondoka ndio inakuwa imekwisha hakuna kingine utakachoweza kufanya. Hivyo basi nikukumbushe tena usikubali kuacha kutumia nafasi yoyote inayokuja mbele yako ambayo inakuwezesha wewe kufika kule unakotaka. Usikubali kukata tamaa na kusema haiwezekani na wakati bado upo hai.

Nakutakia Kila La Kheri.

Kupata huduma na Bidhaa mbalimbali kwenye mtandao huu bonyeza linki hii www.jacobmushi.com/kocha

Makala hii imeandikwa na Kocha Jacob Mushi. Mwandishi wa Vitabu na Makala, Kocha wa Maisha, na Mjasiriamali.

526; HEKIMA: Sumu Niliyowekewa Kwenye Chakula.

“Ilikuwa ni siku za mwisho wa mwaka ambapo tulikuwa na utaratibu wa kwenda kuwasalimia ndugu na jamaa ambao hatujawaona miaka mingi.

Katika kuwatembelea ndugu jamaa na marafiki wengi siku moja nikapitia kwa ndugu mmoja ambaye hatukuonana muda mrefu sana.

Huyu ndugu baada ya kunipokea alinisisitiza sana nile chakula. Nilimkatalia kwasababu nimepita nyumba nyingi na nimeshakula.

Lakini kwa maneno yake matamu nikajikuta nakubaliana nae. Akaniwekea chakula kingi kweli.

Tulikuwa tumekaa nje chini ya mti mkubwa wa mwembe, pembeni yangu nilizungukwa na kuku mwenye vifaranga aliekuwa anatafuta chakula.

Wakati nasubiria mwenyeji huyu aniletee maji ya kunawa ili nile chakula kile nikaona si vibaya nikiwatupia hawa vifaranga chakula kidogo tu (ulikuwa wali).

Wakati naendelea kusubiria maji ya kunawa akapita mtu kwenye njia iliyopakana na nyumba ya mwenyeji wangu. Akanisalimia nilikuwa nimemsahau kabisa. Kumbe nilisoma nae shule ya msingi.

Nikaondoka chini ya mwembe ule kwenda kumfata kwa karibu, wakati huo mwenyeji wangu hajaleta maji sijui ni nini kilimchelewesha.

Kumbe wakati naondoka yule kuku mwenye vifaranga akarukia juu ya kiti nilichoweka chakula akakimwaga na akaendelea kula na wanawe. Nikageuka kurudi kumfukuza lakini chakula chote kilimwagika.

Nikasema labda huyu kuku ndie alitakiwa ale hiki chakula. nikaendelea na kusalimiana na yule ndugu. Akaondoka, wakati narudi na mwenyeji nae alikuwa anakuja na maji. Kumbe chakula kuku ameshakimwaga.

Akasema anakwenda kunipakulia kingine, nikamkatalia nikamwambie ulinilazimisha sana ndio maana kimemwagika.

Tukaagana nikaondoka.

Kumbe Baada ya kuondoka masaa kadhaa baadae nakuja kuambiwa yule kuku pamoja na vifaranga wake wote walikufa.

Chakula nilichotakiwa kula kiliwekwa sumu ambayo ingeniua taratibu.

Mungu ni mkubwa sana akaniokoa na kifo, kwa namna ya ajabu.”

Nataka ujifunze hapa kitu kikubwa katika maisha yako rafiki.

Kuna amengi hutokea kwenye maisha tunayaona kama ni mabaya au ni mikosi lakini wakati mwingine ni mipango ya Mungu kutuokoa na tusivyoviona.

Unaweza kuachwa na gari kumbe uliokolewa na ajali mbaya.

Unaweza kuachwa na mpenzi kumbe umeokolewa na tatizo la maisha.

Unaweza kutengwa na ndugu kumbe ni ili uweze kukutana na watu watakaoweza kukusaidia.

Hakuna kitu kinatokea kwa bahati mbaya, yule mwenyeji wangu hakuchelewa kuniletea maji kwa bahati mbaya japo ningeweza kumlaumu.

Yule ndugu niliesoma nae aliepita akasababisha chakula kumwagwa na kuku hakupita tu kwa bahati mbaya. Alipita kwa kusudi maalumu. Huenda alikuwa apite mahali pengine lakini akasukumwa kupita njia ile bila hata yeye kujua.

Yule kuku na vifaranga vyake sio kwamba walishindwa kwenda kutafuta chakula shambani, hapana walikuja pale chini ya mwenye kwa kusudi la Mungu la kuniokoa.

Lolote baya linalotokea kwenye maisha yako usiwe mwepesi kulalamika, tafakari jiulize ni kwanini haya yanatokea. Ni kwa kusudi lipi?

Kuna mengine yatatokea leo ili tu uje utimize kusudi miaka 20 ijayo.

Musa hakuwekwa kwenye kisafina bahati mbaya, alikuwa anaandaliwa.

Yusufu hakuchukiwa na ndugu zake bahati mbaya yalikuwa ni makusudi maalumu ambayo yalikuja kuonekana miaka kadhaa mbele.

Wewe unapitia ugumu leo unakata tamaa, unapitia changamoto fulani leo unakata tamaa. Ndoto zako unaacha kuzifuatailia kumbe yale yanayotokea yanakuandaa kuelekea kwneye ndoto na kusudi lako.

Nataka Ujifunze kwenye kila kitu kinachotokea kwenye maisha yako kila siku.

Nakutakia Kila La Kheri.

Kupata huduma na Bidhaa mbalimbali kwenye mtandao huu bonyeza linki hii www.jacobmushi.com/kocha

Makala hii imeandikwa na Kocha Jacob Mushi. Mwandishi wa Vitabu na Makala, Kocha wa Maisha, na Mjasiriamali.

525; HEKIMA: Ni Wewe.

Ni wewe utawajibika pale unapoingia kwenye matatizo bila kujali ni nani aliyeyasababisha.

Ni wewe utatakiwa kuchukua hatua pale mambo yanapokuwa magumu kwasababu ya uzembe unaoufanya sasa.

Ni wewe utakalipa gharama za ulaji mbovu unaokula sasa pale utakapoanza kusumbuliwa na magonjwa.

Ni wewe utakaelipa gharama ya ujinga unaoundekeza sasa hivi, unaambiwa ujifunze hutaki,

Unaambiwa uweke akiba unapuuza kwasababu sasa hivi unapata kila unachokitaka.

Unaambiwa ujenge tabia za mafanikio hutaki, unaona wewe hakuna wa kukuelekeza kwasababu tayari unakila unachotaka.

Ni wewe utakaewajibika kwa lolote litakalotokea kwenye maisha yako kutokana na uzembe au kwa namna yoyote ile.

Wale uliokuwa unawaona hawana maana wakati wakikushauri watakutoza fedha ukiwarudia kwenda kuwaomba ushauri tena.

Wale uliokuwa unaona kama wanafuatilia maisha yako, hawajielewi, wenyewe hawana maisha kama yako kwa hivyo hawawezi kukushauri chochote utawafata kwa gharama kubwa.

Sikutishi nakwambia ukweli, ile gharama unayokwepa kulipa sasa hivi utakuja kuilipa siku moja huko mbeleni, bahati mbaya sana utailipa na riba.

Kama unaona ni ngumu sana sasa hivi kuweka akiba kwasababu pesa zipo za kutosha ipo siku utaingia gharama ya kukopa mambo yakiwa mabaya.

Ni wewe ndiye utakaewajibika kwa makosa yako, sisi tutaendelea kubaki kama washauri tu.

Ni muhimu kuchukua hatua sasa kwasababu hata ukikwepa lazima utakuja kulipia gharama kwa kile ulichokikwepa.

Nakutakia Kila La Kheri.

Kupata huduma na Bidhaa mbalimbali kwenye mtandao huu bonyeza linki hii www.jacobmushi.com/kocha

Makala hii imeandikwa na Kocha Jacob Mushi. Mwandishi wa Vitabu na Makala, Kocha wa Maisha, na Mjasiriamali.

524; HEKIMA: Panda Mti

Katika kutafakari sana siku ya leo juu ya Maisha yetu hapa duniani, nimekutana na jambo hili la ajabu sana. Nasikia kabisa Mungu anasema nikwambie, nizungumze na wewe ambaye umekata tamaa katika sehemu mbalimbali za Maisha yako.

Unajua unaweza kufanya vitu vya aina mbalimbali vyote vikaharibika bila kukuletea mafanikio yoyote. Njia rahisi unaweza kuchagua ni kukata tamaa na kujiona wewe huwezi chochote. Sasa leo nataka ukafanye jambo hili la muhimu sana kwenye Maisha yako na dunia kwa ujumla.

Umefikia mahali unaona wewe hujawahi weza kukaa kwenye mahusiano yakadumua hata siku moja. Nenda Katafute mti unaoupenda sana Uoteshe (Panda Mti)

Umefikia mahali unaona kila biashara unayofanya unafeli yaani hujawahi kabisa kupata mafanikio kila ukijaribu unashindwa.

Otesha Mti.

Umejaribu njia mbalimbali kutafuta mtoto na hadi sasa hujapata.

Otesha Mti.

Umefikia Hatua unataka kujiua kwasababu unaona hakuna anaekupenda.

Nenda Kapande mti unaoupenda uwe unauhudumia.

Watu wanasema wewe hutaolewa tena umri umeenda.

Nenda Kaoteshe Mti.

Kila unachokifanya kinaharibika.

Otesha Mti.

Unajiona wewe hakuna cha maana ulichofanya hapa duniani.

Otesha Mti.

Ndio inawezekana kuna mengi unapitia kwenye Maisha na umefikia mahali unasema sasa mimi nimechoka kabisa.

Katafute tunda la mti unaoupenda uoteshe uanze kuuhudumia.

Kama hujaweza hata kufanya chochote cha maana kule kwenu na unaona aibu hata kurudi nyumbani.

Tafuta muda nenda Otesha mti wa matunda na uwaambie wauhudumie na kuupenda kama ambavyo wangekufanyia wewe.

Kuna mtu ulimpenda sana na imeshindikana kuwa nae. Nenda kaoteshe mti uutunze na kuuhudumia vizuri kama vile ambavyo ungefanya kwa yule uliekuwa unampenda.

Umempoteza mpenzi wa Moyo wako kwa kifo (Pole Sana). Nenda kaoteshe Mti.

Miaka 10 ijayo mti huu uliootesha leo utakufundisha kitu kikubwa sana kwenye Maisha yako kama bado utakuwa hai. Kama hautakuwepo hai basi utakuwa ni alama kubwa kwa wale uliowaachia.

Embu jiulize ukijiua sasa hivi kwasababu Maisha ni magumu au ukatoroka na kutelekeza familia utakuwa umeacha alama ya aina gani?

Ukiotesha mti ambao unaweza kuupata bure au kununua mche kwa gharama ndogo sana mti huo unaweza kuja kuwa alama kubwa sana kwa wale unaowapenda.

Ipo siku watakula matunda ya mti huo na watakukumbuka. Ipo siku watakaa kwenye kivuli cha mti huo na watakukumbuka.

Usiseme wewe huwezi kitu bado una kitu unaweza kufanya na kikaacha alama hapa duniani. Usiojione wewe kila unachokifanya basi hakiwezekani naamini ukiotesha mti utaota. Ukiotesha mti utaweza kuuhudumia hadi ukakua.

Sasa Rafiki yangu wewe ambaye kuna kitu umekuwa unakitafuta kwa muda mrefu bila ya mafanikio hapa duniani naombe ukaoteshe mti. Mti huu uwe ni alama kwa niaba ya kile ulichokuwa unakitafuta. Endapo utapata ulichokuwa unakitafuta mti huu utakufundisha uvumilivu, endapo utakikosa basi mti huu utakuwa umeacha alama kwa kile ulichokuwa unakitafuta.

Usikubali kusema huwezi, unaweza kuotesha mti na mti huo ukawa alama kubwa sana hapa duniani.

Kupata huduma na Bidhaa mbalimbali kwenye mtandao huu bonyeza linki hii www.jacobmushi.com/kocha

Makala hii imeandikwa na Kocha Jacob Mushi. Mwandishi wa Vitabu na Makala, Kocha wa Maisha, na Mjasiriamali.

523; HEKIMA: Uzima Ni Fursa

Kuna mtu yupo hospitali anamlilia Mungu ampe uzima ulionao, halafu wewe ni mzima na unakata tamaa.

Jacob Mushi

Unapotaka kukata tamaa kumbuka kwamba kuna watu ambao wanalilia nguvu ulizonazo sasa hivi. Kuna mtu anaipigania pumzi ya mwisho ili angalau aendelee kuwa hai.

Nataka ujue kwamba uzima ulionao ni fursa kubwa sana kwasababu ni nafasi ya kujaribu tena. Ni nafasi ya kujifunza kwenye makosa uliyofanya.

Kuna watu wamefanya mambo wakakosea na kukosea kwao kukawa sababu ya kupoteza maisha. Wewe ulie mzima unakubalije kusema huwezi kufanya tena.

Kila siku mpya unayoiona ni nafasi nyingine tena ya kuchukua hatua mpya, kujifunza vitu vipya, kukutana na watu wapya kwa ajili ya kesho yako.

Usikubali kuridhika na hatua ambayo umefikia sasa hivi, usikubali kuendelea kubakia kwenye hatua uliyofikia sasa. Tumia uzima ulionao kuchukua hatua ya kusonga mbele.

Kesho yako ipo mikononi mwako, kesho yako ipo kwenye uzima ambao umepewa.

Kupata huduma mbalimbali ninazotoa tembelea kwenye link hii www.jacobmushi.com/huduma

Nakutakia Kila la Kheri

Rafiki Yako

Jacob Mushi.

515; Sehemu 3 Muhimu sana za Kuwekeza kwenye Maisha Yako Kila Siku.

Hello Rafiki yangu, leo ni siku ya kumi yam waka 2020 siku zinaendelea kukatika bado kidogo tutasikia mwaka upo nusu. Je bado waendelea kusubiria kidogo ndio uanze kufanya mambo yako? Rafiki yangu utachelewa sana kama hutakuwa mtu wa tofauti.

Mwaka mpya bila ya akili mpya mtazamo mpya, hakuna kitakachobadilika. Aya ngoja niachane na hayo usije ukajisikia vibaya ukaacha kusoma.

Leo nimekuandalia Makal kuhusu sehemu 3 za Muhimu sana kuwekeza kwenye Maisha yako kila siku. Hizi ni sehemu ambazo inawezekana hujawahi kufahamu kwamba uwekezaji unahitajika. Watu wengi wakisikia uwekezaji hufikiria Zaidi mambo ya fedha, hisa, mashamba, majengo n.k. lakini kumbe kuna sehemu nyingine. Kwenye Makala hii utakwenda kuziona vizuri.

Jana nimeandika Makala inahusu kuwekeza Tsh 40,000/= (elfu arobaini) halafu ikurudishie tsh 400,000/= ndani yam waka mmoja (Unaweza kuisoma kwa kubonyeza maneno haya.). kuna watu waliisoma na hawakuelewa vizuri sasa kwa kupitia Makala hii ya leo utaweza kufahamu vizuri Zaidi.

Ukweli uwekezaji Upo sehemu Zaidi ya moja na watu wenye mafanikio hupenda kutuambia kwamba tuwekeze Zaidi kwenye akili zetu, maana yake kuwekeza kwenye akili ni sehemu nyingine pia ya kuwekeza. Wewe unavyosoma Makala hii kujifunza unawekeza pia, kuna vitu utavifahamu vitakusaidia leo au miaka kumi ijayo. Uwezo wa kusoma ulionao hukujua leo uliwekeza kwenye elimu na sasa kwa kupitia elimu unaweza kuvuna matunda sasa hivi.

Sasa nisikuchoshe twende kwenye hizo sehemu tatu muhimu sana kwenye Maisha yako kuwekeza kila siku.

a/ Uwekezaji kwa Kupitia Kipato/Mali.

Hapa tunazungumzia uwekezaji unaotokana fedha au mali ambazo mtu anamiliki. Wewe unalipwa mshahara wa milioni mbili kwa mwezi basi ukaamua uwe unawekeza Tsh laki tano katika ule mshahara wako kwenye uwekezaji wa aina mbalimbali mfano ukanunua HISA, ukanunua mashamba, ukaanza ujenzi wa nyumba za kupangisha n.k. huu uwekezaji umezoeleka sana na mtu anaposikia kuhusu uwekezaji anaelewa moja kwa moja ni mambo haya.

b/ Uwekezaji Ndani yako.

Hapa sasa tunaingia kwako wewe binafsi, tunagusia AFYA, AKILI, NA ROHO YAKO. Ukisikia mtu ana matatizo ya presha au kisukari au uzito ulipitiliza mara nyingi sababu zinakuwa huyu mtu alishindwa kuwekeza kwenye afya yake. Alishindwa kuupa mwili vyakula vyenye afya kwa ajili ya Maisha ya baadae. Sasa kuwekeza kwenye afya ni kutengeneza afya bora ambayo itakuwezesha wewe uweze kuishi vizuri miaka 10,20, 50 ijayo.

Kuwekeza kwenye akili yako ni kuhakikisha unajilisha maarifa ya kutosha ili uweze kuleta mabadiliko kwenye Maisha yako baadae. Kuna vitu unaweza kujifunza leo vikabaki vinakuingizia faida Maisha yako yote yaliyobakia.  

Pia Kuwekeza kwenye Roho hapa ni kujenga mahusiano bora kati yako na Mungu. Najua unaamini Mungu yupo. Sasa kama hutawekeza kwake unafikiri mwisho wako utakuja kuwaje? Siku ukiondoka utakwenda kumwambia nini?

Yule mtu ambaye unataka kuwa hatokei tu kiarahisi inahitajika nguvu kubwa katika kuwekeza ndani yako. Lazima uhakishe unakuwa na AFYA BORA, MAARIFA NA HEKIMA hivi vitakusaidia kuwa mtu bora ambaye ana mchango mkubwa kwenye Maisha yako na wengine.

c/ Uwekezaji kwa Wale Uwapendao/Ndugu/Marafiki na Jamii.

Huu ni uwekezaji kwa wale unaowapenda na kwa jamii inayokuzunguka. Hapa kwa wewe ambaye una mke/mume/Watoto/ndugu na marafiki utapaswa kufanya kitu kwa ajili yao.

Vile vile utapaswa kufanya kitu kwenye jamii inayokuzunguka. Sio lazima ukifanyacho kiwe ni kinahitaji fedha bali kiwe ni kitu chenye kuongeza thamani na kinachogusa Maisha yao. (Jamii inaweza Kuwa Mtaa Unaoishi/ulikotoka, kanisani/msikitini unakosali.).

Kwa kupitia kuwekeza kwa hawa watu miaka ijayo utakuja kuyaona matunda ya uwekezaji wako. Utazungukwa na jamii ambayo inatokana na uwekezaji wako kwao. Utaishi Maisha ya furaha kwasababu uliweza kuitengeneza jamii ambayo ulikuwa unaitaka.

Mke/mume/Watoto hawawezi kuwa vile unavyotaka kama wewe hujachangia. Badilisha kile unachowekeza kwao kila siku. Maneno yako unayoongea nao ni uwekezaji, vile unavyowatendea ni uwekezaji miaka michache ijayo watakuwa kile ulichokuwa unawafanyia.

Sasa jiulize wewe umepambana tu kuwekeza kwenye fedha ukaisahau jamii, kukaibuka kizazi cha watu katili sana. Hawa watu watakuja kukudhuru wewe au wale unaowapenda. Lakini ukiwekeza japo kwa kuwaonesha upendo na kuwajali utajiepusha na madhara.

Haya Rafiki tayari nimegusia sehemu tatu za Muhimu kuwekeza kwenye Maisha yako kila siku. Nimeadnaa Program inaitwa WEKEZA CHALLENGE 2020 ambayo tutakuwa tunayalenga maeneo haya matatu kwa mwaka huu 2020 na kuendelea. Itakuwa vyema sana ukijiunga kwasababu itakusaidia kuwa mtu bora sana.

Ili kujiunga na program hii yakupasa kulipa ada ambayo ni Tsh 40,000/= kwa mwaka mzima. Kujiunga Unaweza kulipa ada moja kwa moja kwenye namba za Tigopesa 0654 726 668 au Mpesa 0755 192 418 majina yanatokea Jacob Moshi. Baada ya kulipia Nitumia ujumbe kwenye WhatsApp namba 0654 726 668 wenye majina yako na neno WEKEZA.

Karibu Sana

Rafiki Yako

Jacob Mushi.

514; HEKIMA YA LEO Upendo Ni Amri

Siku zote amri inapotolewa kinachofuata huwa ni Utii na unaposhindwa kutii amri maana yake wewe unakuwa muasi. Kwa serikali zetu ukiasi kinachokujia ni hukumu wakati mwingine hata kifo kutegemea na yule aliekupa amri.

Sasa tukisoma kwenye neno la Mungu Yohana. 13:34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Maana yake kupendana na ndugu zako, watu waliokuzunguka, ni amri sio ombi, sio kitu unabembelezwa ufanye; kinyume chake sasa ukichukia wewe unakuwa muasi unakuwa umeiasi amri hii ya upendo.

Huwezi kusema unampenda Mungu usiomwona wakati unamchukia ndugu yako ambaye unamwona.

Kwanini tunapaswa kuhimiza upendo?

Bila ya Upendo Hakuna Amani.

Bila ya Upendo hakuna furaha.

Bila ya Upendo Hakuna maendeleo.

Bila ya Upendo tutaishia Kuuana tu.

Kama humpendi mtu huwezi kufurahia mafanikio yake, huwezi kuhamasika na mafanikio yako, huwezi kujifunza kwa yule unaemchukia. Jifunze kupenda wengine ili uweze kujifunza kwao.

Yeye alitupenda akautoa uhai wake kwa ajili yetu na mpaka sasa kuna mabilioni ya watu wanamtumikia. Hivyo basi ili wewe uweze kupokea upendo kwa wengine hakikisha unatoa upendo. Hata kwa wale wanaokuchukia hakikisha unawaonesha upendo.

Soma: Kristo Angeondoka Bila Ya Kuzungumzia Kurudi mara Ya Pili Ingekuaje?

Hata wale waliokutendea ubaya wa kila namna waoneshe upendo. Kwa kufanya hivyo utajitengenezea njia bora ya mafanikio kwenye Maisha yako.

Tafakari sasa hivi ni mtu gani ambaye ukimfikiria unasikia uchungu? Kwanini unaendelea kuubeba uchungu ndani yako? Naomba leo umwambie nimekusamehe, nimekuachilia, halafu uendelee na Maisha yako.

Wapo wengi wamekutendea mambo mabaya sana hata hayafai kuelezea hadharani kwasababu yanaweza kukufanya uchafuke najua inauma sana, najua imekua doa kubwa sana. Embu jiulize yeye alieteswa uchi msalabani bila ya kosa lolote angekufa bila ya kusamehe ingekuaje? Wewe inakuaje unashindwa kusema Nimewasamehe Nawapenda sana wale walionitendea mabaya.

Upendo Pekee ndio Kisasi cha kweli.

Nakutakia Kila la Kheri

Rafiki yako

Jacob Mushi.

512; Mimi Ni Mtenda Dhambi Kuliko Wewe.

Siku Moja nilikuwa nawaza hivi, “Siku Nikifa Nikakuta hakuna Mungu Nitacheka Sana”, Sauti nyingine ndani yako Ikasema, “Hapo Utakapokuwa Unachekea ni Nani Huyo Atakuwa Amekutengenezea” Ndugu Yangu Mungu Yupo, Ukatae Ukubali…………………

Kuna ule mtazamo wa kuwaona watu ambao wamefanya mambo makubwa, na wale wenye ushawishi mkubwa sana kuwa hao ni watu wasio na makossa kabisa. Na hiyo hupelekea pale wanapokosea kitu cha kawaida kabisa mfano ndoa kuvunjika, tunawaona kama vile ni wamefanya makossa makubwa sana.

Wakati huo huo kuna watu wengi sana kila mara ndoa zao zimekuwa na matatizo makubwa na wanaishia kuachana bila hata kujulikana.

Rafiki napenda ufahamu kwamba kila mmoja ana jambo ambalo huwa ni udhaifu wake. Kila mmoja kuna kitu ambacho kimekuwa kinamshinda mara kwa mara hata wewe ukijitafakari utaona kunai le dhambi ambayo kila mara hukuangusha. Hata kama hakuna anaeijua basi wewe mwenyewe na Mungu wako ndio mnaijua vizuri.

Kama kwako kuna kitu kama hicho basi ina maana kwamba kila mtu kuna jambo ambalo limekuwa likimsumbua pia. Kila mmoja kuna ka udhaifu Fulani huwa kinamwangusha. Ndio maana katika wanafunzi 12 wa Yesu bado kulikuwa na mmoja Yuda Iskariote aliemsaliti Yesu kwa tamaa ya fedha. Bado pia kuna Petro ambaye alimkana Yesu mara tatu, kuna mwingine huyu anaitwa Thomaso alishindwa kabisa kuamini kama Yesu amefufuka mpaka amshike kwa mikono yake.

Sasa kama Yesu mwenyewe alijua amechagua watu 12 wazuri na bado wakaonekana wenye madhaifu mimi ni nani niseme sina dhambi hata kidogo? Ndio maana nataka kukwambia mimi ni mtenda dhambi kuliko wewe, Neema ya Mungu tu ndio hunisaidia, napenda ulijue hili ili usije kunihukumu siku moja ukisikia makosa niliyoyatenda. Vilevile hata wewe kuna kitu najua ni udhaifu wako, unakusumbua mara kwa mara, umekuwa unajaribu kuacha lakini unakwama.

Nataka uwe na mtazamo chanya kwenye mambo ya wengine uweze kuchukuliana na kila mtu kwasababu kila mmoja ana jambo ambalo linamsumbua sana ndani yake hata kama hatakwambia. Na haya mambo ndio mara zote huwaga ni siri za ndani ya watu.

Unaweza kuwa unasema sasa Jacob unataka kusema kila mmoja awe huru kufanya dhambi ile ambayo inamshinda? Hapana hapo utakuwa umenielewa vibaya, maana yangu hapa ni kuwa wewe utambue mtu akiwa hai na akakosea kwa chochote kile bado ana nafasi ya kutubu mbele za Mungu wake.

Inawezekana Mtu ametenda uovu ukasambaa sana akatubu kwa Mungu akapata msamaha na wewe ukaendelea kumhukumu, kumsema vibaya, kumuandika vibaya, ikatokea umekufa ukaenda kuhukumiwa kwa kutenda dhambi ya kuhukumu wengine. Maana yangu hapa kama wewe huna nafasi ya kwenda kumshauri au kumsaidia mtu aliekosea usipoteze muda wako kumsema na kumzungumzia kwasababu huenda unasema yule ni mtenda dhambi sana, kumbe alishatubu siku nyingi na kusamehewa.

Hakuna haja ya kuzungumza mabaya ya mtu kama huwezi kuzungumza mazuri yake. Hakuna haja ya kumchukia mtu alietenda maovu bali twapaswa kumuombea Mungu amsaidie. Na wewe binafsi ukishaujua udhaifu wako basi ni jukumu lako, kuhakikisha unakaa mbali na vile vitu ambavyo vinakupelekea kuitenda dhambi. Ukishatambua kile ambacho kinakuangusha kirahisi ni jukumu lako kutafuta msaada kwa watu wenye uwezo kwenye tatizo lako wakusaidie uweze kujidhibiti.

Rafiki Yako Jacob Mushi.

511; Unakimbilia Wapi? Tazama Pembeni Yako.

 Haya Ndio Maisha yetu kwenye vitu vingi tunavyopitia kila siku, Soma kisa hiki ujifunze: “Habari kaka Jacob, ninaomba ushauri wako kuhusu hili. Ni mwaka wa tatu sasa tangu nikutane na binti mmoja na nikampenda sana. Nina tabia moja huwa sikati tamaa haswa pale ninapokuwa nimekipenda kitu Fulani maishani mwangu. Nimekuwa naamini kwamba ipo siku tu kitakuwa cha kwangu.

Binti huyu kila nilipokuwa namfuatilia ili niweze kuwa nae amekuwa akinisumbua sana, kila wakati ananipiga chenga za namna mbalimbali. Nimejitahidi kumpatia kila anachokitaka, lakini alikuwa anasema anatamani tuwe marafiki tu kwani tukiingia kwenye mahusiano tutakuwa tunagombana na mwisho wake tutaachana.

Kwasababu nilimpenda kwa dhati ikanibidi nimsikilize tu. Sasa huu ni mwaka wa tatu tumekuwa karibu kama marafiki na nilijiapiza sitaingia kwenye mahusiano mengine kwakuwa niliona kama ananipima uaminifu wangu.

Wiki mbili zilizopita kanijia huku akilia machozi na kuniomba msamaha anasema ananipenda sana na yupo tayari kuwa na mimi kuanzia sasa. Anadai amegundua alikuwa anapoteza muda na watu ambao hwakuwa wanampenda bali kumtumia tu.

Hilo halikuwa shida, kubwa Zaidi ananiambia kwamba mwanaume aliekuwa nae kwenye mahusiano kwa Zaidi ya miaka 3 akijua anampenda, amempa ujauzito na kumkimbia. Huku akidai hawezi kuwa nae kwenye Maisha yake.

Naomba ushauri wako, nifanyeje, ukweli huyu binti nampenda sana, changamoto ni huu ujauzito alioniletea, sielewei kama ananipenda kweli au ni kwasababu ya matatizo aliyopitia tu. “

Kijana huyu amekumbwa na mkasa huu mzito sana kwenye Maisha yake. Ni kweli inaumiza sana, nataka na wewe ujifunze kitu kwenye huu mkasa, je ni vitu gani umekuwa ukivikimbilia ukijua ni vyako mpaka pale ulipopoteza?

Huyu binti amekua akishikamana na watu ambao hawakumpenda na akasahau kabisa kuona mtu aliekuwa karibu yake wakati wote. Inawezekana hata wewe kuna vitu umekuwa unavishikilia ukidhani ni vyako na ukasahau vile ambavyo ni vyako siku zote vipo karibu na wewe siku zote.

Embu jaribu kutazama ni nani huwa yupo karibu yako kila mara? Ukiwa na shida, ukiwa na raha yupo. Wakati wowote ukimhitaji anakuwa yupo tayari kwa ajili yako. Naomba nikwambie watu hawa ni wa thamani sana kwenye Maisha yetu. Usikubali kuwa mtu ambaye unaiona thamani yao wakati wa matatizo tu.

Kuna watu wanaweza kukwambia wanakupenda kwa maneno matamu lakini kuna watu wanakupenda kwa kufanya vitendo kwenye Maisha yako. Kuna watu ambao hujawahi kusikia wakisema NAKUPENDA lakini wamekuwa wakifanya mambo makubwa kwenye Maisha yako kuliko neno hilo na NAKUPENDA.

Jifunze kutofautisha watu wanaouhitaji mwili wako na wanaouhitaji moyo wako, jifunze kutofautisha watu wanaozihitaji pesa zako na wanaokuhitaji wewe kwenye Maisha yao. Wapo wengi wanaonekana kama wanatuhitaji sisi kumbe wanahitaji vile vitu tulivyonavyo. Ukishindwa kujua haya utaishia kutumbukia kwenye shimo kila mara.

Rafiki Yako

Jacob Mushi.

KITABU: NUKUU ZA MAISHA.

Nukuu za Maisha (Malengo, Mafanikio, Mahusiano n.k) ni Kitabu kinachokupa muongozo wa maneno ya kutafakari kila siku asubuhi ili uweze kuwa na siku bora na yenye mafanikio.

Kitabu hiki kina nukuu 400+ ambazo zinakupa uwezo wa kufikiri vizuri, kuishi kwa furaha na kuweza kusonga mbele katika kile unachokifanya.

Nukuu za Maisha ni mjumuisho wa nukuu za furaha, nukuu za mahusiano, nukuu za upendo, falsafa za maisha, nukuu za mafanikio, nukuu za biashara, nukuu za hamasa, nukuu za malengo, nukuu za kutia moyo, nukuu za kuongeza ujasiri, nukuu za kuongeza kujiamini na kadhalalika usiache kusoma kitabu hiki.

NUKUU ZA MAISHA ni mkusanyiko wa nukuu ninazoandika kwenye mtandao wa Instagram kila siku. Nimezikusanya zaidi ya 400 na utaweza kuzisoma kwenye kitabu kimoja.

SHUHUDA ZA NUKUU HIZI KWENYE MAISHA YA WATU

Hakika nimesoma maandiko yako mengi sana nimepata mafanikio makubwa sana kifikira sasa nimeweza kukaribia malengo niliyojiwekea Mungu akutie nguvu. Pia baada ya kumaliza kusoma kitabu cha USIISHIE NJIANI nimejifunza mambo mengi sana.

EvaStella Ricknelson

Tangu nimeanza kufuatilia NUKUU za Jacob kwenye mitandao ya kijamii nimeona mabadiliko makubwa, nimekuwa jasili, najiamini, napambana sana kwenye utafutaji wangu, na nimejifunza kuto kukata Tamaa.

– Stella Samwel

 Katika nakala zako na jumbe zako zimenifungua macho maana Nilikuwa sioni wapi ninapokwenda katika maisha yangu yapo Mambo mengine niliyaona hayawezekani lakini leo nayaona yanawezekana.

Elisha Dismas

Ni kweli nimepata vitu vingi toka kwenye nukuu zako za Maisha! Ukweli ni kwamba maisha halisi ni Maarifa, uko vizuri, zidi kutafuta maarifa utaishi ndoto zako pia ukimtanguliza Mungu mbele maana Zawadi na vitu vingine vyote vyatoka kwa MUNGU

Justin Kabembo

 “Tangu nimeanza kufuatilia NUKUU za Jacob kwenye mitandao nimeona mabadiliko makubwa kwenye Maisha yangu. Kwanza nimeamini maisha ni kuthubutu. Pili kila jambo linaanzakufanikiwa katika akili yako. Tatu, Matendo yako yanakuwezesha kutengeneza ile picha uloifikiria kuwa halisi. Nne, rafiki/mchumba/mke/mume ni chachu ya mafanikio au changamoto za mafanikio yako. Hivyo chagua maisha!!

Joshua S. Lebabu

Tangu nimeanza kufuatilia Makala zako nimekuwa nikipata maneno mazuri ya faraja ya kutokukata tamaa katika safari ya mafanikio

Prosper Cosmas

Tangu nimeanza kusoma nukuu na vitabu vya jacob Mushi. Nimepata mwanga mkubwa sana nimekuwa mtu mwenye upeo na maono makubwa kimafanikio, japo ni katikati lakini angalau nimekuwa mfano wa kuigwa. Isitoshe Jacob amenishauri mambo mengi ya kimaisha na kibiashara. Ni miongoni mwa waandishi bora hapa nchini. Hakika huwezi Jutia ukisoma nukuu na vitabu vyake.

Denis Tesha

Tangu mwaka 2016 nilipoanza kukufuatilia umenifanya niwe mtu mpya Na niweze kufanya mambo ambayo sikutegemea kuwa yanafanyika.

Baraka MWAMPULULE

“Kwakweli nukuu zako zinatoa mwanga mpya na kutia moyo kwa walioanguka wainuke na kuendelea.”

Mtaalam Md

Kwanza kabisa namshukuru Mungu kukuleta maishani kwangu Kaka, hakika umekua sehemu ya mabadiliko katika nyanja tofauti tofauti maishani mwangu, Vitu vingi Sana nimejifunza na ninazidi kujifunza kutoka kwako, umenifundisha ujasiri wa kuthubutu, umenifundisha namna ya kuyatumia matatizo Kama fursa ya kuingiza kipato, namna ya kuishi na watu, ni  mambo mengi sana, Hadi mda huu naona utofauti mkubwa Sana katika maisha yangu tofauti na nilivyokuwa mwanzoni, ubarikiwe Sana na uzidi katika Hilo.

Peter Mahunja.

Nimejifunza Ni jinsi gani ninaweza kujisimamia binafsi.

Kareem

Tangu nimeanza kusoma kazi zako, Vitabu na kwa blog pamoja na nukuu nimejifunza vingi vya kunipa hamasa ya kusonga mbele na zimechangia kubadilisha maisha yangu kifikra kwa kiasi kikubwa.

Peter Mbizo

Binafsi mimi makala zako zimenifanya niwe mtu wa kujiamini na kufanya kila kitu bila kukata tamaa na kuwa mtu subira maana Hapo mwanzo nilikuwa mtu wa wasiwasi na muoga wa kujaribu kufanya kitu asante sana kwa makala zako za kutia moyo.

Nelson Frank Mushi.

Hata pasipo ya kuniuliza ni mabadiliko gani nimeweza kuyapata kupitia kufuatilia nukuu hizi ningelikuambia siku moja kuwa ama hakika wewe ni nabii ulikubalika kwenu. Nukuu zako zimenijenga sana katika swala la kutokujikatia tamaaa kulingana na hali za maisha niyoyaishi kila siku ni hii ni baada ya kusoma jarada lako moja kuhusu maisha ya Daud pamoja na wazazi wake hadi kuufikia ufalme.

Steven Samwel

Nashukuru mno Bro kwa kweli Mimi ni mdau wako namba moja, mafundisho yako yanafariji na kukufanya mtu ujitambue, Kama Kuna sehemu ulisinzia basi ghafla unaamka, mie ni single mom kwa hiyo Niko na changamoto nyingi ninazopitia katika kujikwamua, Kuna muda nakuwa na stress ghafla nikikusoma naona Kama wasema Mimi, basi napata funzo na kupiga hatua nyingine.

Rehema Lebby

 

Tangu nimeanza kusoma kusoma kitabu chako nimejitambua kwa kweli nimejifunza kuwa na mimi ninaweza kufanya jambo nikaweza kwa uelewa wangu nilionao, nimejifunza ni aina gani za marafiki natakiwa kuwa nao, ni mambo gani inabidi niyafanye ili niweze kutimiza maono yangu kwa kweli hiyo ni kwa ufupi lakini nimejifunza mengi na bado naendelea kuyatendea kazi.

Nuriath Nuru

Kiukweli bila kuficha toka nianze kufuatilia nukuu zako ndugu jacob mushi kuna mabadiliko makubwa kwangu. Kwanza kwasasa, najiamini, Sina hofu, Nathubutu, Siahirishi mipango, Nimekuwa na nidhamu Asante sana kwa nukuu zako.

Wille Balisho

Nadhani kila mtu hapa Duniani anahitaji mtu wakumtia moyo, inawezekana maneno ya mtu yakatosha nikiwa nasoma najitia moyo kwa maneno yako nakusonga mbele bila kuishia njiani.

Palmaraham Nkya

NAMNA YA KUPATA KITABU HIKI:

Bei ni Tsh 10,000/= hardcopy/softcopy,

Namba za Malipo.

0654 726 668 Tigopesa. Jacob Moshi,