Unaweza kujikuta unafanya mambo hayaendi kabisa na wala huoni matokeo yake unayoyataka kwasababu  upo nje ya kusudi la Mungu.

Mungu  hajakuumba kwa bahati mbaya ulikuja kwa kusudi na upo hai ili utimize kusudi. Hakikisha unalitambua kusudi la Mungu maishani mwako ili uweze kuishi maisha yenye furaha na baraka za Mungu.

Hujazaliwa duniani ili uje kuzaa peke yake. Dunia ina watu wengi wa kutosha tayari. Unaweza kufanya mambo ya kawaida au kulifanya kusudi la Mungu ndani yako.

Hakikisha unachokifanya kinaongeza thamani ya maisha ya wengine. Kama kinawaumiza watu hakiwezi kumfurahisha Mungu.

Tawi lisilozaa hukatwa na kutupwa motoni. Lakini kabla halijakatwa huachwa kwa muda na kupaliliwa ili kuangalia labda litazaa na wewe Mungu amekupa nafasi ya kujitafakari leo kwanini uendelee kuishi wakati huna unachoongeza duniani.

Ni wakati wako wa kutimiza kusudi  unaweza kuanza leo haijalishi una miaka mingapi sasa. Yesu alitumia miaka mitatu tu kufanya lililomleta duniani. Hata wewe unaweza kuanza leo.

Tenga muda wa kutosha kama lisaa limoja peke yako jiulize: Kwanini nipo hai mpaka leo? Ni kitu gani Mungu anataka nikitimize? Tafakari kwa kina muulize Mungu wako atakuonyesha.

Haupo hai kwa bahati mbaya.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading