Katika vitu ambavyo hatuwezi kuvibadili katika maisha yetu ni historia huwezi kubadili tena vile vitu ulivyowahi kuvifanya jana,  juzi na miaka iliyopita.  Kitu cha muhimu ni wewe  kuweza kugundua kwamba ulikosea wapi na uanze kutumia wakati huu ulionao sasa kufanya yaliyo sahihi.

 Hata uwe umefanya mabaya kiasi gani huwezi kuyafuta huwezi kubadili chochote unatakiwa utambua kuwa hiyo ni historia na isikufanye wewe ushindwe kutumia vyema siku hizi za pekee ulizopewa bure. Haijilishi umefanya biashara ngapi zikafeli umekosea mara ngapi,  hiyo sio sababu ya wewe kushindwa tena leo. Leo ni zawadi ambayo ukiweza kuitumia vyema utafanya mambo makubwa sana kuliko ulivyokosea.

Isamehe jana samehe makosa uliyoyafanya samehe kila ulichokosea na uanze upya. Katika vitu ambavyo hatuongezewi ni muda wote tunapewa masaa 24  na kila mmoja ana matumizi yake juu ya muda huo tumia vyema muda wako uweze kuacha historia njema duniani.

Siku moja tu inatosha kubadili kila kitu ulichowahi kukosea. Siku moja inatosha kufanya mambo makubwa inategemea tu wewe unaitumiaje siku yako. Ukitumia siku yako kufikiria jinsi ulivyoshindwa kwenye biashara utaipoteza,  Ukitumia siku yako vyema kufikiria juu ya baadae yako hapa duniani na kufanya vitendo utaweza kusonga mbele. Haupo hai kwa bahati mbaya Mungu ana kusudi na kuwepo kwako yapo majukumu hujamalizia. Uhai wako ni fursa ya kubadili historia mbaya ya maisha.

Ni wakati wako wa kutengeneza historia mpya ya maisha yako fursa ya kwanza uliyonayo ni pumzi, una afya njema, una muda mwingine tena leo.  Acha kulalamika, kulaumu, fanya majukumu yako kwa bidii na maarifa,  Jifunze kila siku, Lazima utapata matokeo yaliyo bora.

Asante sana na Karibu
©Jacob Mushi 2016
 Niandikie 0654726668 Whatsapp  E-mail jacob@jacobmushi.com

2 Responses

  1. Kaka Nakukubali Sana mzee umekuwa mwalimu wangu kila siku unachopost kinanibadili akili na mtazamo wangu, Nimepata mwanga wa kutosha sana kupitia elimu unayoitoa kupitia post zako, naomba uniruhusu nitakapokwama Nikupigie tuongee na unifundishe zaidi na zaidi. Mimi Ni King Mushi rafiki yako fb

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading