Nilikua nazungumza na mchekeshaji mmoja nikawa namuuliza maswali haya; Tunasikia wewe ni tajiri umewezaje kua na pesa wakati unafanya kitu cha kawaida sana cha kuchekesha watu?
Akajibu akaniambia; Kadiri watu wanavyocheka ndivyo ninavyotengeneza hela” Nikamuuliza; unafanyaje ili watu waendelee kucheka kila wakati maana wasipocheka hutengenezi pesa! Akaniambia; ili watu wacheke Zaidi naongeza thamani ya vile ninavyoviongea!
Nikajifunza kwamba haijalishi unafanya kitu gani ili uweze kuongeza kipato chako njia rahisi na ya kwanza ni kuongeza thamani yako. Kabla hujafikiria kuanzisha biashara nyingine anza kwanza kuongeza thamani yako. Kabla hujafikiria kwenda kusoma ili upandishwe cheo bado unaweza kuongeza thamani yako na ukapandishwa cheo.
Badala ya kutumia mwili wako ili upate kazi au uongezewe mshahara wewe binti ongeza thamani yako watakutafuta wenyewe. Badala ya kwenda kwa waganga ili bidhaa zako zitoke sana ongeza thamani ya bidhaa zako na utoaji huduma wateja watakuja wenyewe. Ili nyimbo zako zisikike Zaidi na ziguse maisha ya wengi usiishie kumwomba Mungu peke yake ongeza thamani ya kile unachokiimba watu watatafuta CD zako.
Ili upate wafuasi wengi ongeza thamani ya maneno yako watu watakufuata. Watu wanafuata thamani siku zote sio kingine.
Sikuishia hapo nikamuuliza na swali linguine ambalo ni la muhimu sana nilimuuliza naongezaje thamani yangu? Akaniambia thamani yako itaongezeka kwa kufanyia kazi kile unachokifanya, kujifunza kila siku, kusoma vitabu, kusikiliza sauti za kuhamasisha, na Kuangalia video za mafunzo. Kisha yale unayojifunza niyaweke kwenye kile ninachokifanya.
Jitazame leo kabla hujalalamika mambo hayaendi sawa kipato ni kile kile jiulize Unastahili kuongezewa? Unachokitoa kinalingana na kile unachotaka kupata? Ili uongezewe mshahara usitumie muda mwingi sana kwenye maombi tumia muda mwingi kwenye kuongeza thamani yako kazini. Ili upandishwe cheo usipoteze muda wako kujipendekeza kwa bosi ongeza thamani yako kwa kujifunza sana juu ya kile unachokifanya.
Jim Rhon anasema Tunalipwa kutokana na thamani tuyapeleka kwa watu. Hivyo angalia kwanza unasababishaje watu wakulipe kabla hujaanza kulalamika na kulaumu.
Ili watu wakufuate tumia muda mwingi kufanyia kazi vile vilivyoko ndani yako siku hadi siku utaanza kuona matokeo yake.
Karibu sana.
Kingdom of Success
0654726668
Jacob Mushi
www.mushijacob.info

3 Responses

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading