TUKUMBUSHANE TU JUU YA SUALA ZIMA LA MAGONJWA YA ZINAA.

By | December 28, 2018

Habari wapendwa nichukue nafasi hii kuongelea juu ya swala zima la magonjwa ya zinaa. Labda tujiulize Magonjwa ya zinaa ni nini? Magonjwa ya zinaa ni magonjwa ambayo yanasambazwa kwa njia ya vitendo vya kijinsia yakiwemo kaswende,kisonono,klamidia,kankroidi,utando mweupe n.k .Magonjwa hayo yamekua tatizo kubwa hasa katika taifa letu la Tanzania ni kutokana na changamoto mbalimbali ambazo watu wanapitia kwa namna tofautii.

Je unawezaje kuwa katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa?

Jkuna njia mbalimbali hatarishi ambazo zinaweza kumpelekea mtu akapata magonjwa ya zinaa njia hizo ni kama zifuatazo;

  • Njia kubwa ni kujihusisha na vitendo vya ngono hatarishi,ninapoongelea juu ya suala zima la kitendo cha ngono hatarishi ni ngono isiyo salama hasa na yule mwenye maambukizi ya zinaa
  • Biashara ya kujiuza, hii pia kwa namna moja ama nyingine imekua sababu za watu kupata maambukizi ya magonjwa hayo kiurahisi
  • Kuwa na wapenzi  wengi, jambo ambalo sio salama kwani kuna uwezekano mkubwa wa usambazaji wa zinaa kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine
  • Ulawiti na rushwa ya ngono , tatizo hili limewakumba wengi katika nchi yetu na katika taasisi mbalimbali kwani wengi wao wamekua wakifanya hivyo ili tu kuweza kupata fidia juu ya jambo fulani au kupewa kipaumbele kwa namna ambayo sio sahihi.
  • Kuanza michezo ya ngono bado umri mdogo;vijana wa sasahivi wameharibikiwa kutokana na vitu wanavyoviona mtanadaoni na mwisho wake huwa wanaishia kufanya kama yale wanayoyaona.

Hizo ni baadhi za njia ambazo magonjwa ya zinaa yanaweza kuenea kwa urahisi zaidi,ila pia vilevile tunahitaji kujua nini kifanyike kuzuia janga hilo ambalo limekua tatizo kubwa katika jamii.

Je unawezaje kuepukana na hatari ya kupata maambukizi ya zinaa?

   Unaweza kuepeuka kupata magonjwa ya zinaa endapo;

  • Ukiwa mwaminifu kwa mpenzi mmoja.
  • Ukichukua hatua kali kwa uongozi wa juu kwa kupiga vita dhidi ya rushwa ya ngono na ulawiti.
  • Epuka ngono isiyo salama tumia kondom.
  • Piga vita dhidi ya biashara haramu za miili.

Madhara yake katika jamii ni nini?.

Hivyo basi kutokana na magonjwa haya kuwepo kwa asilimia kubwa  kumefanya watu wengi kuwa na huzuni  hasa katika kupata watoto imekua ni tatizo kwani magonjwa  haya yamekua ni visababishi  vya wanawake na wanaume wengi kukumbwa na janga la kuharibikiwa na mfumo wao wa uzazi hivyo basi kutowesha furaha na kuleta huzuni ndani ya ndoa au mahusiano.Pia vilevile magonjwa hayo yamekua pia ni changamoto kubwa katika kurudisha maendeleo ya jamii kwani yamepoteza nguvu kazi kwa asilimia kubwa kutokana na kupotea kwa kizazi/uzao. Lakini vilevile magonjwa ya zinaa kwa upande mwingine yamefanya baadhi ya watu katika jamiii kujiona hawafai na kujiona wenye fedheha kwa namna moja au nyingine mbele ya jamii.   

Nini kifanyike?

Nitaongelea kitu kimoja juu ya magonjwa haya, magonjwa haya yasiwe sababu ya wewe kukata tamaa na kujiona hufai katika jamii kwani magonjwa haya ni kama magonjwa mengine yanatibika na kuepukika . Hivyo basi mpendwa msomaji wa makala hii  chukua hatua dhidi ya magonjwa hayo kwani yanatibika na kupona haraka endapo ukiwahi tiba na kuishi kadri ya vile impendezavyo  Mungu.

Ubarikiwe sana,

Rafiki yako, Kocha Audrey Lugusi

www.jacobmushi.com/kocha.

2 thoughts on “TUKUMBUSHANE TU JUU YA SUALA ZIMA LA MAGONJWA YA ZINAA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *